Sambaza:

KATIKA kuongeza kasi ya kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi mbalimbali kwa ufanisi zaidi na kukuza soko nchini, ZoomTanzania imezindua tovuti mpya kwa watumiaji wa simu za mkononi (smartphones).

Ikiwa ni nyenzo muhimu ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano ya kutaka nchi iwe ya viwanda, uzinduzi huo unaenda sambamba na maendeleo ya sayansi na teknolojia ambapo Watanzania wengi hutumia simu za ‘smartphones’ katika biashara zao.

muonekano mpya wa zoomtanzania

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mtaalamu wa tovuti ya ZoomTanzania, Terence Silonda, alisema tovuti hiyo mpya ni ya kipekee kwani imeboreshwa zaidi kwa kuwa na logo mpya, tovuti itapatikana katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza na imewezeshwa kwa ajili ya simu za mkononi (smartphones).

“Kwa kuwa zaidi ya asilimia 67 ya Watanzania wanatumia simu za mkononi ambazo nyingi ni ‘smartphones’ kuuza au kununua bidhaa na huduma nyinginezo kupitia tovuti ya ZoomTanzania.com, tovuti hii itawarahisishia zaidi kwa kuwa imefanyiwa mabadiliko makubwa. Zoom ni tovuti ambayo iliwezeshwa kwa ajili ya simu ndogo za mkononi pekee (feature phones).

Baada ya kugundua kuwa watumiaji wengi wa simu hutumia ‘smartphones’, tukauongezea uwezo mfumo wa ZoomTanzania ili kurahisisha watumiaji kuweka bidhaa zao katika tovuti kiurahisi zaidi na pia kuwasiliana na muuzaji kiurahisi zaidi,” alisema.

Mengineyo yaliyoboreshwa katika tovuti ni pamoja na machaguo mengi wakati wa kutafuta vitu, ukubwa wa maandishi umeongezwa, Whatsapp plugin itakayowezesha mtumiaji kusambaza taarifa zake haraka zaidi, blog iliyojawa na hadithi nzuri na za kuvutia.

SOMA NA HII:  Airtel ni mali ya TTCL Palifanyika Mchezo wa Hovyo - Rais John Magufuli

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Zoom- Tanzania, Kirk Gillis, alisema Zoom imepiga hatua zaidi katika mapinduzi ya teknolojia ya tovuti kwa miaka zaidi ya sita sasa.

“Tovuti hii imebuniwa kwa ajili ya soko la Tanzania, tunajua na tunasikiliza watumiaji wetu. Uzinduzi huu ni mwanzo tu mengi zaidi yanakuja kutoka kwetu,” alisema. Akizungumzia maboresho ya baadaye, alisema kuanzia mwakani wamepanga kupanua wigo mpana katika mtandao wa Zoom kwa kuwaunganisha wanunuzi na wauzaji wa bidhaa mbalimbali. ZoomTanzania ni tovuti inayoongoza Tanzania kwa matangazo ya biashara kupitia mtandao.

Inahusisha biashara 7,500, watumiaji waliosajiliwa zaidi ya 200,000 na ikiwa inatembelewa hadi mara 40,000 kwa wastani wa siku. Ni tovuti inayoaminika zaidi katika kuunganisha wanunuzi na wauzaji nchini Tanzania.


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako