ZIP code ya Tanzania ni ipi? Fahamu masuala ya ZIP code


Ikiwa umechanganyikiwa kwa muda mrefu kuhusu ZIP code sahihi ya Tanzania, basi chapisho hili ni kwa ajili yako, kwa sababu linatoa ufafanuzi.

ZIP code

Kwa taarifa yako, ZIP (Zone Improvement Plan) codes hutumika kwa Marekani tu.  Marekani haitumii nambari za posta (postal codes) kutoka nchi nyingine kama “ZIP” codes.

Katika nchi nyingine zote, nambari za posta zinatumika. Hata hivyo, ZIP codes kwa Marekani hutumiwa kwa malengo sawa na nchi nyingine zinazotumia postal codes – kwa ajili ya masuala ya mailing.

SOMA NA HII:  Goal Technology kuanza kutumika kwa mara ya kwanza Afrika

Kwa hiyo, ZIP codes ni kwa Marekani wakati utambulisho wa posta (postal codes) ni kwa nchi nyingine – ikiwa ni pamoja na Tanzania.

Hata hivyo, kumbuka kwamba USPS (United States Postal Service) ina codes kwaajiri ya nchi nyingine, ambazo hutumiwa wakati wa kushughulikia utumaji wa mizigo. Nambari hizi ni sawa na ZIP codes zinazotumiwa ndani ya Marekani. Nambari ya Tanzania ni 00171-2000.

Unaweza kutembelea tovuti hii Complete Domestic and International ZIP Code Numeric List kufahamu ZIP codes za nchi nyingine.

Sasa, unawezaje kujaza fomu zinazoomba utumie ZIP code?

Ikiwa unajaza fomu mtandaoni, na inataka ujaze ZIP code yako, weka tu 00255 au 35091. Baadhi ya Tovuti zinaweza kukataa codes zote mbili. Katika kesi hiyo, jaribu 00176. Angalau moja ya codes hizi inapaswa kufanya kazi.

SOMA NA HII:  TTCL Kusimamia Njia Mpya ya Malipo kwa Wateja wa Mwendokasi

Usifanye kosa hili, tafadhali …

Usiingize 255 kama ZIP code ya Tanzania. Hii ni nambari ya kupiga simu ya kimataifa ya Tanzania. (Kila unapohitajika kuingiza ZIP code, tumia 00255, 35091, au 00176.)

Ikiwa makala hii imekusaidia, tafadhali shirikisha na wengine.

One Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA