Sambaza:

Kununua kompyuta iwe laptop au desktop huwachanganya watu wengi hasa wasiokuwa na uzoefu wa vifaa hivi maana ukifika dukani utakuta za kila namna na miundo tofauti, Nimeona niandike makala hii kuwasaidia wale wanunuaji wapya wapate muongozo ili angalau wanapokwenda dukani wajue wanataka nini.

MAMBO YA KUZINGATIA

 • MatumiziUnapotaka kununua kompyuta, jambo la kwanza ni kujua unataka kwa ajili ya matumizi yapi? kuna watumiaji ambao wao ni kufungua mitandao ya kijamii , kusoma barua pepe tu na kufanya kazi zake ndogo ndogo hawa wanahitaji kompyuta zisizo na sifa (Specifications) kubwa, kuna ambao wanafanya , video editing hawa wanahitaji mashine zenye uwezo mkubwa.

 

 • BeiHapa ndiyo muhimu, utakuta mtu anataka kompyuta yenye sifa kuubwa mfano ram Gb 6, au processor quad core, hard disk 400 GB kuendelea halafu unakuta ana kiasi kidogo cha pesa, kama huna hela ya kutosha sio tatizo, unaeza ku upgrade kidogo kidogo baadae ukipata hela, mfano nunua ram GB1 then baadae utaongeza mpaka zifike hata 6 kwa kompyuta inaruhusu, au hard disk kama ni ndogo unaweza nunua kisha siku za baadae ukaongeza.

 

 • Mfumo wa uendeshaji (OS)  :Angalia mahitaji ya mwisho ya hiyo kompyuta unayonunua, mara nyingi uwa imeoneshwa kuwa hiyo pc imeundwa kwa ajili ya mfumo  gani wa uendeshaji, zipo kwa ajili ya ubuntu, zipo windows XP, 7, 8 n.k
SOMA NA HII:  Je, Unapenda Laptop Aina Gani ?

 

 • Ukubwa wa umbo: Baadhi ya watu kama mimi napenda screen kubwa kama desktop haina kuanzia inch 22 au laptop ianzie inc 15 uwa sina raha maana mimi ni mpenzi wa movies na games, jambo la muhimu ni kuwa screen kubwa ni nzuri kwa wale wenye macho yenye udhaifu, ila kuna ambao wanapenda vile vidogo vidogo labda kwa sababu ni rahisi kubeba nakadhalika.

 

 • Matundu (ports) : Kutokana na mahitaji yako, angalia kompyuta ambayo itafaa ukiwa umeweka flash pia unaweza kuweka modem, printer nakadhalika, siku hizi kuna hdmi connection, kuna usb 2 na usb 3 ports, matundu kwajili ya intaneti.

 

 • Jina: Baadhi ya watu kwa sababu moja au nyingine atakwambia amnapenda HP au Dell au Samsung au Toshiba, mfano unaponunua pc ya Hp au samsung unapewa warant ikizingia unaweza irudisha ukatengenezewa au ukapewa mpya.

 

 • Uhifadhi (Hard Disk) :  uhifadhi wa ndani wa kompyuta ni uwezo wa kifaa chako kuhifadhi vitu mbali mbali kwa watumiaji wa kawaida sio tatiuzo sana hii, ila kwa watumiaji wakubwa (wale wanopenda kudownload softwares mfano adobe suit uwa zina mpaka 5GB)  wale wapenzi wa kudownload movies, games , na wengineo wanahitaji hard disk kubwa. Magwiji wa kompyuta huulizia SATA au SCSI drives.

 

 • RAM: Kwa watumiaji wadogo sio ishu sana hii, hata ram ya 2Gb ni kubwa kutosha matumizi yake yoote, Ila watumiaji wakubwa hasa wale professionals wangependa kutumia kuanzia 4 – 6 GB. pia operating systems kama windows 32bit na 64bit zina minimum requirements za Ram itakayotumika kuziendesha.wataalam wa kompyuta wenyewe wakati wa manunuzi huulizia DDR2 au DDR3.
SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuongeza Nafasi Kwenye Kompyuta

Kwa leo tuishie hapa, kama umepata chochote hapa kifanyie kazi maoni ushauri acha comment yako hapo chini.


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

This article has 1 comment

 1. Amani Reply

  Asante sana kwa uchambuaji mzuri kwa kuwezesha kupat akompyuta ambayo inaweza kukidhi mahitaji yetu

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako