Zinazosomwa App Kutoka Tanzania Inayoonesha Mambo Yanayovuma


Zinazosomwa ni app inayokusogezea habari unazopenda kuzisoma kutoka vyanzo vikubwa mbali mbali Tanzania. Kwa mfano kama wewe unapenda tu kupata habari za michezo na burudani, basi app hii itakupa habari za michezo na burudani tu! Kama unapenda habari za siasa basi itakusogezea habari za siasa tu. Vileviel kama unapenda habari zote zile basi itakuletea habai zote!


App hii ina uwezo wa kugundua ni jambo gani au mtu gani maarufu anavuma Tanzania katika siku. Hili linawezekana kwani app hii ina uwezo wa kukusanya habari kutoka kwenye blogs na news sites maarufu Tanzania zaidi ya 35. Inazichambua habari hizi na kugundua jambo gani au mtu gani anatrend Tanzania.


Pia app hii inapangilia habari katika topic au mada mbalimbali kama siasa, michezo, burudani, uchumi n.k ili kumrahisishia msomaji. Hii inasaidia mtumiaji kusoma habari ambazo anapenda kuzisoma.

App hii inapatikana google play kupitia link hii Zinazosomwa – Applications Android sur Google Play na inaambatana na website yake www.zinazosomwa.com ambayo inafanya kazi hiyo hiyo.


Malengo ya App hii:

1. Kumrahisishia mtanzania kupata habari

2. Kuwaongezea waandishi wa habari idadi ya wasomaji

Chanzo: www.zinazosomwa.com, T3RN3K,  Google Play

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA