Zimbabwe kutumia teknolojia ya alama za vidole kwenye uchaguzi wake 2018


Serikali ya Zimbabwe imetangaza kuwa imeingia mkataba wa kusambaza vifaa na teknolojia ya kutambua alama za vidole (fingerprint biometric) na kampuni ya Marekani, Ipsidy.

Vifaa na pamoja na programu zitakazozuia mtumiaji kupiga kura zaidi ya mara moja kwa kutumia alama za vidole vitasambazwa na Ipsidy itajumuisha Mfumo wa Utambulisho wa Kidole (Automatic Fingerprint Identification System) ambao utatumika katika uchaguzi ujao wa 2018 nchini Zimbabwe.

Kampuni ya Ipsidy ilichaguliwa baada ya kushinda zabuni ya kimataifa ili kusambaza vifaa vya kupigia kura na teknolojia husika. Mkataba huo ulisainiwa na kamisheni ya uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC)

“We are very pleased to have been selected by the ZEC to provide this critical solution, ahead of all competitors under the tender. This award represents the continued recognition of the efficacy and value of Ipsidy’s identification platform, software, and services in the African election market,” said Thomas Szoke, Chief Technology Officer at Ipsidy.

Ipsidy inasema itaunganisha daftari la wapiga kura na teknolojia ya AFIS, ambapo itapatikana orodha na idadi kamili ya wanaostahili kupiga kura kwenye uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika siku zijazo mwaka huu. Database ya wapiga kura ya zimbabwe ilianzishwa mwaka 2017 na imekuwa ikitumika kujua watakaostahili kupiga kura kwenye chaguzi mbalimbali.

Uaminifu wa orodha ya wapiga kura utazingatiwa na usahihi wa taratibu za uchapishaji na taratibu za kukata rufaa.

Tangazo la uteuzi wa Psidy linakuja miezi michache baada Raisi Robert G. Mugabe kujiuzulu kama rais nchini Zimbabwe ambae amehudumu kwa miongo kadhaa katika nafasi hiyo. Mugabe alikuwa akituhumiwa kuchakachua matokeo ya uchaguzi kila mara.

Ipsidy ina makao makuu huko New York na ina matawi ya uendeshaji huko Colombia na Afrika Kusini.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *