Home Nyingine Zaidi ya watu 30 wameuawa na maporomoko ya taka Addis Ababa, Ethiopia.

Zaidi ya watu 30 wameuawa na maporomoko ya taka Addis Ababa, Ethiopia.

0
0

Zaidi ya watu 30 wameuawa na maporomoko ya taka kwenye eneo moja kubwa la kumwaga taka nje ya mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.

Watu zaidi ya 150 walikuwa eneo hilo, watu wengine bado hawajulikani waliko tangu maporomoko hayo yatokee siku ya Jumamosi usiku.

Eneo hilo limekuwa likitumiwa kutupa taka kutoka kote mjini Addis Ababa kwa zaidi ya miongo mitano. Watu wengi wamekuwa wakitumia eneo hilo kujitafutia riziki huku wengine wakiwa ni wenyeji .

Mpaka sasa bado mabanda kadha ya watu yamefukiwa chini ya taka.

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *