YouTube Imeingia Kwenye Deal Kubwa na Label za Muziki


youtube

YouTube imesaini makubaliano mapya ya muda mrefu na kampuni mbili kubwa za usimamizi wa kazi za wasanii wakubwa duniani, pia imeahidi kuimarisha sheria zaidi za kupakia (uploads) kwa watumiaji wanaoweka nyimbo zenye hakimiliki na kutengeneza njia ya huduma mpya ya kulipia baada ya majadiliano ya miaka miwili.

Universal Music Group imesema mpango wake na YouTube utawawezesha wasanii kubadilika na kulipwa vizuri zaidi. Sony Music Entertainment pia imesaini mkataba mpya.

Mkataba huo umeanzisha viwango vipya vya malipo (royalty) kati ya YouTube na mashirika yenye hakimiliki za video za muziki na clips zinazopakiwa na mtumiaji, hii imefungua njia kwa YouTube kuanzisha huduma mpya ya kulipia kwajilli ya muziki, huduma hii inatarajiwa kuanza kufanya kazi mapema mwakani -2018 . Warner Music Group, kampuni ya tatu kwa ukubwa kwenye sekta ya muziki, ilisaini mkataba mpya na YouTube mwezi Mei.

SOMA NA HII:  Baada ya kashfa thamani ya facebook yashuka kwa $58bn

YouTube inatarajia kubadili baadhi ya mamilioni ya watu ambao husikiliza muziki bure kwenye tovuti yao ya video kuwa wanachama wanaolipia. Hiyo itasaidia kuimarisha uhusiano wake na makundi makubwa ya kampuni za usimamizi wa wasanii baada ya mvutano wa miaka mingi kuhusu kama tovuti hiyo inayomilikiwa na Google inalipa kiasi cha kutosha kwa wamiliki wa hakimiliki.

Universal, inayomilikiwa na Vivendi SA, ilipata udhibiti kwa mara ya kwanza juu ya kile kinachoonekana kwenye channels zinazoruhusu matangazo na kuishawishi YouTube kuboresha skanning kwa upakiaji wa mtumiaji unaojumuisha maudhui yenye hakimiliki, inasemekana baadhi ya nyimbo na video zitapatikana kwenye huduma ya kulipia tu.

YouTube ni mojawapo ya njia ambayo watu duniani kote hutumia kupata muziki, na mojawapo ya nyenzo muhimu kwajili ya kujitangaza. Hata hivyo tovuti hiyo na kampuni mama ya Google, kitengo cha Alphabet Inc., wamekuwa wakipata shida kuwashawishi watumiaji kulipia muziki.

SOMA NA HII:  Tech!! Apps 8 Unazoweza Kuzitumia Kugeuza Windows Pc Kuwa Wi-fi Hotspot

Kampuni kubwa za muziki sasa zitahamishia jitihada zao kwa Facebook Inc., mmiliki wa mtandao mkubwa zaidi wa kijamii. Facebook imekuwa ikizungumza na kampuni za muziki kwa zaidi ya mwaka kuhusu licensing rights kwa video zinazowekwa na watumiaji, na, ikiwezekano, video za kitaalamu pia.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA