Yanga Yavutwa Shati Na Zanaco March 11 2017, Full Time 1-1

Comment

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika, Yanga( Dar es Salaam Young Africans) wameshindwa kutamba katika mchezo wa kwanza dhidi ya Zanaco ya Zambia uliofanyika Jumamosi ya March 11 2017 Jijini Dar es salaam.

Yanga iliwachukua dakika 38 kuandika goli la kwanza kupitia kwa Simon Msuva akiifungia goli la kuongoza akipokea pasi ya Justine Zulu, katika Dakika ya 82, Atram Kwame aliisawazishia Zanaco wakitumia mwanya wa kutokuwa na maelewano baina ya mabeki wa Yanga.

Mpaka dakika tisa zinamalizika Yanga 1-1 Zanaco ambapo mechi ya marudiano inatarajiwa kuwa kati ya Machi 17-19.

Up Next

Related Posts

Discussion about this post

error: Content is protected !!