Yanga SC Yakwea Pipa Kuifuata MC Algier, Chirwa aachwa

Comment

Yanga inaondoka kesho saa 12 jioni kwenda Algeria ikipitia Dubai huku ikimkosa nyota wao raia wa Zambia Obrey Chirwa.

Yanga inakwenda kucheza mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho dhidi ya MC Alger ambayo ilikubali kipigo cha bao 1-0 jijini Dar.

Kitakuwa kikosi cha watu 20 bila ya mshambuliaji wao Obrey Chirwa ambaye imeelezwa ana matatizo ya kifamilia.

Wachezaji wengi wanaokosa mechi hiyo ni Ally Mustapha ‘Barthez’, Pato Ngonyani, Justine Zulu, Yusuf Mhilu na Anthony Matheo.

Up Next

Related Posts

Discussion about this post