Kwaheri !! Yahoo Sasa Haipo Tena

Yahoo haipo tena na Mkurugenzi Mtendaji wake, Marissa Mayer amejiuzulu.

Mayer ambaye hivi karibuni alipokea dola milioni 23 ‘golden parachute’ kwa ajili ya kazi yake kwenye kampuni hiyo, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Yahoo tangu 2012. Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni za Usalama na Fedha, Mayer alikuwa anamiliki hisa za Yahoo karibu dola milioni 4.5, ikiwa ni pamoja na chaguzi na vikwazo vya hisa, kwa hivyo atakuwa ameondoka na karibu dola milioni 260.

Verizon hivi karibuni imetangaza kuwa imekamilisha kuinunua Yahoo kwa dola bilioni 4.48. Kampuni hiyo ina mipango ya kuchanganya huduma za Yahoo na zile za AOL katika tawi la kampuni ya Verizon linalotambulika kwa jina la Oath. Oath , ambayo ina zaidi ya media 50 na bidhaa zingine za teknolojia, itakuwa inaongozwa na Bwana Tim Armstrong aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa AOL kabla ya hii.

Wakati huo huo, sehemu ya biashara za Yahoo zilizobaki ambazo ni hisa zake katika kampuni kubwa ya kufanya manunuzi mtandaoni(e-commerce) kutoka China- Alibaba na ushirikiano wake katika Yahoo Japan, itaendelea kuwepo kama kampuni tofauti iliyopewa jina la ‘Altaba Inc’, Mkurugenzi Mtendaji wa Altaba kuanzia Juni 16 ni Thomas McInerney , ambaye alikuwa CFO wa “Barry Driller IAC”. Kampuni pia imehamishia makao yake makuu katika jiji la New York.

SOMA NA HII:  Ifahamu Facebook ya bure kutoka Vodacom Tanzania

Wakurugenzi watano wa bodi ya Altaba watajiuzulu kama sehemu ya kuhitimisha mpango huo, yaani Eddy Hartenstein, David Filo, Jane Shaw, Richard Hill, Maynard Webb na bila shaka, Marissa Mayer.

Hatua hii ya Verizon inaonyesha kama njia ya kupanua uwezo wa kampuni na kufikia watumiaji wengi zaidi.

COMMENTS

WORDPRESS: 2
  • comment-avatar

    Tusibirie kama watarudisha Yahoo kwenye ligi ya kupambana na Gmail na Hotmail/Outlook

    • comment-avatar

      Mimi sidhani kama watakuwa na nguvu ya kushindana na Gmail tena kwa sababu Google wamewekeza nguvu nyingi kwenye mfumo wao wa mail na tayari huduma nyingi mtandaoni zimeunganishwa na mifumo ya google.Ila kubadilishwa kwa uongozi na umiliki kuna weza kuleta mabadiliko na hari mpya kwa Yahoo