Yahoo Imesema Akaunti zote Bilioni 3 za Watumiaji ziliathiriwa na Udukuzi


Yahoo, ambayo kwa sasa ni sehemu ya Verizon Communications Inc, siku ya Jumanne ilisema kuwa uchunguzi ulionyesha kuwa akaunti zake bilioni 3 za watumiaji  ziliathiriwa katika wizi wa data wa mwaka 2013, mara tatu ya makadirio yake ya udukuzi mkubwa wa kihistoria.

Yahoo-mediahuru

Hata hivyo, kampuni hiyo imesema uchunguzi ulionyesha kuwa taarifa zilizoibiwa hazijumuishi nywila katika maandishi ya wazi, data za kadi za malipo, au taarifa ya akaunti ya benki.

Yahoo mwezi Desemba iliyopita ilisema kuwa data kutoka kwenye akaunti zaidi ya bilioni 1 ziliathiriwa Agosti 2013.

Verizon mwezi Februari ilipunguza ofa yake ya awali ya kununua mali za Yahoo kwa dola milioni $350 baada ya mashambulizi mawili ya udukuzi yaliyoikumba kampuni hiyo.

Kukamilika kwa mkataba huo, uliotangazwa kwa mara ya kwanza mwezi Julai, ulikuwa umechelewa kutokana na makampuni hayo kupima athari za tatizo la udukuzi wa data uliofanyika mara mbili kwenye kampuni ya Yahoo mwaka jana. Kampuni hiyo ililipa $ 4.48 bilioni kwa biashara ya msingi ya Yahoo.

Siku ya Jumanne, Yahoo ilisisitiza kwamba takwimu bilioni 3 ikiwa ni pamoja na akaunti nyingi ambazo zilifunguliwa lakini kamwe hazijawahi kutumika au zilitumiwa kwa muda mfupi tu.

Kampuni hiyo imesema ilikuwa inatuma taarifa kwa njia ya barua pepe kwa akaunti za watumiaji walioathiriwa zaidi.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *