Xiaomi Yazindua Mi Gaming Laptop Kwaajili ya Kucheza Game


Ilikuwa Jumanne isiyokuwa ya kawaida linapokuja swala la matukio ya teknolojia, kwa sababu Xiaomi, Huawei, na kisha Apple walizindua aina mbalimbali za bidhaa mpya. Makampuni ya Kichina yalizindua simu janja mpya katika matukio ya China na Ufaransa, huku Apple ikizindua iPad mpya katika mkutano wake huko Chicago ikiwa imelenga elimu zaidi.

Ndiyo sababu sisi kama mediahuru ilibaki kidogo tusahau kuzungumzia bidhaa mpya ambazo hatukuzitarajia kabisa. Inajulikana zaidi kwa simu zake za mkononi ,lakini Xiaomi hutengeneza vifaa vingine vya kuvutia, ikiwa ni pamoja na TV, vifaa, na – kuanzia sasa – laptops za game. Ni kweli, Xiaomi imezindua laptop yake ya kwanza ambayo inalenga wacheza game moja kwa moja.

Hii sio laptop ya kwanza ya Xiaomi. Kampuni hiyo inauza Mi Notebook Air inayokuja katika aina mbili, ikiwa ni pamoja na 12.5-inch na 13.3-inch. Xiaomi Mi Gaming Laptop inatumia Windows 10 na ina skrini ya ukubwa wa inchi 15.6 pia ina uwezo wa kuvutia. Tunazungumzia Intel 7th-gen Core processor, Nvidia GeForce GTX 1060 graphics, 16GB ya RAM, 256GB SSD, na 1TB HDD.

Laptop ina umbo dogo, na inakuja na keyboard inayounga mkono rangi milioni 16, na ina keys tano za ziada kwajili ya gamers kwenye upande wa kushoto ambazo zinaweza kutumika kucheza gemu aina yoyote ile.

Chanzo cha picha: Xiaomi

Ili kupunguza mashine kupata moto, laptop hii inatumia 12V cooling fan, na fan outlets nne. Kama unavyoweza kuona kwenye maelekezo haya, laptop hii ni ya kipekee.

Linapokuja swala la ports, inakuja na USB-A ports tatu, sehemu ya headphone na microphone, na slot ya SD. Kwa nyuma, kuna Ethernet port – ndiyo, hiyo ni jinsi gani kompyuta hii ni ndogo.

Mi Gaming Laptop itaanza kuuza nchini China Aprili 13 kwa Yuan 5,999 (Tsh 2,155,400). Aina nyingine yenye uwezo mkubwa zaidi, ikiwa na 16GB ya RAM na kadi ya graphics ya GTX 1060, itauzwa Yuan 8,999 (Tsh 3,230,700). Hakuna taarifa rasmi ni lini Mi Gaming Laptop itaanza kuuzwa kwenye masoko ya kimataifa, lakini ikiwa Xiaomi ina uwepo rasmi katika soko lako, basi tarajia uzinduzi wake katika miezi michache ijayo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA