WordPress vs. Blogger – Ipi ni Bora? (Faida na Hasara)


Tunaulizwa mara kwa mara na watumiaji wapya kwa nini wanapaswa kutumia WordPress badala ya huduma za blogu za bure kama WordPress.com au Blogger ? Mediahuru ni tovuti yenye rasilimali kubwa kwa watumiaji wapya wa WordPress, hivyo ni dhahiri kwamba tunaipenda WordPress juu ya majukwaa mengine ya blogu (blogging platforms). Katika makala hii, tunalinganisha WordPress vs Blogger kukusaidia kuamua ni ipi bora kwa mahitaji yako. Tutaangalia faida zote na hasara za WordPress dhidi ya Blogger, ili uweze kufanya uamuzi bora linapokuja swala la Blogger dhidi ya WordPress kama jukwaa la tovuti yako.

Muhimu: Tafadhali kumbuka kuwa kulinganisha huku ni kati ya WordPress.org na Blogger yenyewe “self-hosted” , si WordPress.com vs Blogger. Tafadhali angalia mwongozo wetu juu ya tofauti kati ya blog ya WordPress.org dhidi ya ile ya bure ya WordPress.com.

1. Umiliki

Blogger ni huduma ya “blogging” inayotolewa na kampuni kubwa ya Google. Ni bure, ya uhakika zaidi muda mwingi, na inatosha kabisa  kuchapisha vitu vyako kwenye wavuti. Hata hivyo,  haimilikiwi na wewe. Google inaendesha huduma hii na ina haki ya kuifunga, au kufunga upatikanaji wako wakati wowote.

Kwa WordPress, unatumia huduma ya “hosting” kuhifadhi tovuti yako mwenyewe. Upo huru kuamua muda gani unataka kuitumia na wakati unataka kuifunga. Unamiliki data zako zote, na unadhibiti taarifa gani unazoshirikisha.

SOMA NA HII:  Tweet ya Kylie Jenner yashusha mapato ya mtandao wa Snapchat

2. Kudhibiti

Blogger ni huduma nzuri yenye vifaa vidogo vyenye kukuwezesha kufanya kazi fulani kwenye tovuti yako. Mambo unayoweza kufanya kwenye blogu yako ya blogspot ni machache, na hakuna njia ambayo unaweza kupanua ili kufikia mahitaji yako.

WordPress ni programu ya chanzo cha wazi ( open source), kwa hivyo unaweza kuipanua kwa urahisi ili kuongeza vitu vipya. Kuna maelfu ya Plugins za WordPress ambazo zina kuruhusu kurekebisha na kupanua vipengele kama vile kuongeza duka kwenye tovuti yako, kujenga portfolio, nk.

Unapolinganisha WordPress vs Blogger kwa tovuti za biashara, basi WordPress ni chaguo sahihi suluhisho la muda mrefu kwa mmiliki yeyote wa biashara.

3. Kuonekana

wordpress-blogger-ni-bora-faida-hasara

Blogger kwa kawaida inatoa seti ndogo ya templates unazoweza kutumia. Unaweza kubadilisha rangi na mpangilio wa templates hizi kwa kutumia vifaa vilivyojengwa ndani yake, lakini huwezi kuunda mipangilio yako mwenyewe au kufanya marekebisho. Kuna baadhi ya templates zisizo rasmi zinapatikana, lakini templates hizo huwa na ubora wa chini sana.

Kuna maelfu ya mandhari za bure na za kununua kwajili ya WordPress ambazo zinakuwezesha kujenga tovuti zenye muonekano wa kitaalamu. Kuna mandhari za WordPress (WordPress theme) kwa kila aina ya tovuti. Haijalishi tovuti yako inahusu nini, utapata mandhari nyingi zinazovutia ambazo ni rahisi kurekebisha na kuboresha.

SOMA NA HII:  Jinsi Ya Kufuta Akaunti Yako Ya Facebook Moja Kwa Moja!

4. Uwezeshaji

wordpress-blogger-ni-bora-faida-hasara

Kuhamisha tovuti yako kutoka kwenye Blogger kwenda kwenye jukwaa tofauti ni kazi ngumu. Kuna hatari kubwa ya kupoteza SEO yako (search engine rankings (, wanachama (subscribers), na wafuasi (followers) wakati wa kuhama.Ingawa blogger inakuwezesha kuhamisha maudhui yako, data zako zitabaki kwenye seva za Google kwa muda mrefu sana.

Kwa kutumia WordPress, unaweza kuhamishia tovuti yako popote unapotaka. Unaweza kuhamisha tovuti yako ya WordPress kwenye “Host” mpya, kubadilisha jina la kikoa (domain name), au hata kuhamishia tovuti yako kwenye mifumo mingine ya usimamizi wa maudhui (content management systems).

Pia kama unalinganisha WordPress vs Blogger SEO, basi WordPress hutoa njia bora zaidi za SEO

5. Usalama

Kutumia Blogger una faida zaidi ya jukwaa salama la Google. Huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kusimamia rasilimali za seva yako, kuiweka blogu yako salama, au kuunda “backups”.

WordPress ni salama kabisa, lakini kwa kuwa ni ya kibinafsi (self hosted) unawajibika kwa usalama na backups. Kuna Plugins nyingi za WordPress ambazo zinakuwezesha kufanya hivyo kwa urahisi.

6. Msaada

Kuna msaada mdogo unaopatikana kwa Blogger. Wana nyaraka za msingi (documentation) na jukwaa (forum) la mtumiaji. Kwa upande wa msaada, uchaguzi wako ni mdogo sana.

SOMA NA HII:  Akismet ni Nini na Kwa Nini Unatakiwa Kuitumia Kwenye Tovuti Yako

WordPress ina mfumo wa msaada wa jamii mzuri sana. Kuna nyaraka za mtandaoni,community forums, na mazungumzo ya IRC ambapo unaweza kupata msaada kutoka kwa watumiaji wenye uzoefu wa WordPress na watengenezaji. Mbali na msaada wa jumuiya, kuna makampuni mengi yanatoa msaada wa kulipia kwajili ya WordPress.

7. Baadaye

Blogger haijatoa update yoyote kubwa kwa muda mrefu sana. Tumeona Google kuua huduma zao maarufu kama Google Reader, Adsense kwajili ya feeds, na inawezekana na FeedBurner. Maisha ya baadae ya Blogger yanategemea Google, na wana haki ya kuifunga wakati wowote wanavyotaka.

WordPress ni “Open Source software” hii inamaanisha maisha yake ya baadaye hayategemei kampuni moja au mtu binafsi (Angalia historia ya WordPress). Inatengenezwa na jumuiya ya watengenezaji (community of developers) na watumiaji. Kuwa mfumo wa usimamizi wa maudhui maarufu ulimwenguni, maelfu ya biashara ulimwenguni kote wanaitegemea. Maisha ya WordPress ni marefu na yenye kuhakikishia.

Tunatarajia kulinganisha  WordPress dhidi ya Blogger kumekusaidia kuelewa faida na hasara za kila mmoja na kukusaidia kufanya uamuzi sahihi kwa biashara yako.

Ikiwa umeipenda makala hii, tafadhali jiunge na blogu yetu kwa mafunzo zaidi. Unaweza pia kutupata kwenye Twitter na Google+.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA