Kompyuta

Windows smartphone-sync sasa inapatikana kwenye iPhone

on

Kipengele kipya cha Microsoft smartphone-sync, ambacho karibuni kilizinduliwa kwajili ya vifaa vya Android, sasa  kinapatikana kwa watumiaji wa iPhones.

Microsoft walizundua kipengele hiki kwenye Windows 10 Insider Preview ya hivi karibuni

“Jambo hili limezingatia uvinjari wa wavuti katika vifaa vilivyounganishwa,” walisema Microsoft.

Baada ya ku-install Windows 10 build, nenda kwenye Settings > Phone, na uunganishe simu yako.

Kiunganisho kinahakikisha vitu vyako kutoka kwenye simu yako vinaendelea kwenye PC uliyochagua.

Baada ya kuunganisha simu yako, nenda kwenye simu yako na uanze kuvinjari mtandao.”

Unapokuwa kwenye tovuti unayotaka kuiangalia kwenye PC yako, unatumia njia ya kawaida ya kushiriki na shirikisha tovuti kwenye chaguo la “Continue on PC”.

SOMA NA HII:  Dalai Lama azindua app ya bure kwajili ya watumiaji wa iPhone

Mara baada ya kuidhinishwa, itakuomba uingie (sign in) na Akaunti yako ya Microsoft. Ni muhimu kutumia akaunti sawa na unayotumia kwenye PC yako.

Kisha itakuuliza ikiwa unataka “Continue now” au “Continue later”. Ukichagua “Continue now”, tovuti hiyo itafungua kwenye PC iliyounganishwa.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.