Jinsi ya kutumia Windows Keyboard Shortcut Alt + Underline


Hii ni njia nyingine ya mkato ya Windows ya keyboard (Windows keyboard shortcut)  kwajili ya mashabiki wa kuongeza uzalishaji popote pale. Njia za mkato ni amri ambazo zinaokoa muda kwa kufanya kazi ya Windows katika vipindi vidogo – badala ya kutumia mouse yako kwajili ya kubonyeza kipengee cha menyu, kuchagua faili, na kadhalika. Keyboard shortcut hii inaitwa Alt + “underlined letter” shortcut.

Angalia picha katika makala hii.

Jinsi ya kutumia Windows Keyboard Shortcut Alt + Underline
menu bar kwenye Firefox 49 kwajili ya Windows.

Ni snip ya menu bar katika toleo la Firefox 49. Bar ya menyu haipo kwa default katika Firefox, lakini unaweza kuiwezesha kwa kubonyeza icon ya menyu ya “hamburger” na kuchagua Customize > Show/Hide Toolbars. 

Hata hivyo, katika Firefox menu bar utaona jinsi maandishi (kawaida ya kwanza) imepigiwa mstari kwa kila kipengee cha menyu – F katika File, au V katika View, kwa mfano? Hiyo ni sehemu ya uzuri wa njia ya mkato ya Alt.

Unaweza, bila shaka, sogeza mouse yako na bonyeza kila kipengee cha menyu ili kufungua. Au unaweza kuokoa muda kwa kubonyeza kitufe cha Alt kwenye kibodi yako na herufi iliyopigiwa mstari kwa wakati mmoja. Kuona historia yako ya hivi karibuni ya kuvinjari (browsing history), kwa mfano, bonyeza tu Alt key na S, na historia yako inakuja moja kwa moja.

SOMA NA HII:  Orodha ya njia za mkato za keyboard katika Mozilla Firefox

Ikiwa upo kwenye toleo la zamani la Windows kipengele hiki kimejengwa ndani yake na ni automatic, lakini matoleo ya baadaye – kama vile Windows 10 – hayana kipengele hiki kwa default. Juu ya hayo, programu za hivi karibuni zinaondoa bar ya menyu ambayo tumezoea kuiona katika Windows XP na matoleo ya mapema ya Windows.

Hata baadhi ya programu katika Windows 7 zina hii ya kisasa zaidi, muonekano ambao ni “menu-less”. Hata hivyo, bado unaweza kutumia njia ya mkato ya Alt + “herufi” katika Windows 10. Kwenye programu nyingiherufi haija pigiwa mstari tena, lakini kipengele bado kinafanya kazi sawa sawa.

Ili kuwezesha kipengele hiki kwenye Windows 10, andika “ease of” ndani ya Cortana search box kwenye taskbar.

Chaguo lacontrol panel linaloitwa “Ease of Access Center” linapaswa kuonekana juu ya matokeo ya utafutaji. Chagua hilo.

SOMA NA HII:  Format memory card, flash drive (Njia ya kuondoa virus kabisa)

Wakati Control Panel inafungua Ease of Access Center shusha chini na uchague link inayosema Make the keyboard easier to use. Kwenye skrini inayofuata, shusha chini kuelekea kwenye “Make it easier to use keyboard shortcuts” na kisha bofya kisanduku cha kuchagua kilichoandikwa Underline keyboard shortcuts and access keys. Sasa bofya Apply kuhifaadhi mabadiliko yako na kisha unaweza kufunga Control Panel window.

Sasa fungua File Explorer kwa kugonga Windows logo key + E, na hakikisha njia za mkato kwa kugonga Alt + F. Hii inapaswa kufungua menyu ya “Faili” ya File Explorer. Unapofanya hivyo utaona kuwa kila kitu kinachowezekana katika orodha hiyo sasa kina “letter label” karibu pembeni yake. Bonyeza tu herufi karibu na kipengee cha menyu unayohitaji, na kisha uendelee kufuata vitu mbalimbali vya menyu na key taps mpaka kufanya kitu unachotaka kwa kutumia kibodi yako tu.

Hii inafanya kazi sawa kwenye programu zingine kama programu za Microsoft Office kama Word na Excel. Ikiwa unatumia Internet Explorer 11 bado unaweza kutumia kipengele hiki hata kama huwezi kuona bar ya menyu katika programu. Anza kwa kugonga kitufe cha Alt key ili kuonyesha menu toolbar.

SOMA NA HII:  Je Kuna Programu ya Windows Unatamani Kuitumia Kwenye Simu ya Adroid ?

Sasa unaweza kuchagua kipengee cha menu unachotaka kulingana na herufi yake iliyopigiwa mstari – katika mfano huu huna haja ya kubonyeza Alt na herufi iliyopigiwa mstari kwa wakati mmoja.

Watumiaji wenye matoleo mapya ya Windows watahitajika majaribio na programu mbalimbali kwenye PC zao ili kuona ambayo inafanya kazi na njia ya mkato ya Alt + “underlined letter” na ambayo haifai.Unaweza kuepuka Windows Store apps kwa sababu haziungi mkono sifa zinazofanana na programu za jadi za desktop. Watu wengi bado wanategemea programu za desktop hata hivyo suala hili halipaswi kuwa jambo kubwa kwa wengi. Mbali na hilo, Microsoft inaweza kuongeza vipengele zaidi kwenye programu zaWindows Store katika miaka ijayo.

Ninapenda kutumia keyboard shortcuts; Mara tu utakapo ona zinaokoa muda kiasi , najua na wewe utaliona hilo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA