Jinsi ya Kusafisha “Windows Desktop” ili Kuongeza Kasi ya Kompyuta


Jinsi ya Kusafisha "Windows Desktop" ili Kuongeza Kasi ya Kompyuta-mediahuru
Ikiwa kompyuta yako zamani ilikuwa inafanya kazi kwa haraka sasa imeshuka na umegundua hilo, angalia kwa karibu desktop yako. Je! Imejaa icons, screenshots na faili? Kila moja ya vitu hivi huchukua “memory” ambayo kompyuta yako inaweza kuiweka kwenye matumizi bora zaidi mahali pengine. Ili kuongeza kasi ya kompyuta yako, safisha Windows desktop.

Je! Kuna Faili Ngapi Kwenye Desktop yako?

Kila wakati Windows inapofunguka, operating memory hutumiwa kuonyesha faili zote kwenye desktop na kupata nafasi ya mafaili yote yanayowakilishwa na njia za mkato (shortcuts.)

Ikiwa kuna faili mengi yamekaa kwenye desktop, hutumia operating memory kubwa, kimsingi kwa madhumuni yasiyo na maana au faida. Kwa kuwa na memori ndogo, kompyuta inaanza kwenda polepole kwa sababu inatakiwa kubadilishana habari kutoka kwenye operating memory hadi kwenye kwenye hard drive. Inafanya mchakato huu-unaoitwa memory paging-kuweka kila kitu mtumiaji anachotaka kutumia kifanye kazi kwa wakati mmoja.

SOMA NA HII:  Format memory card, flash drive (Njia ya kuondoa virus kabisa)

Safisha Desktop yako

Suluhisho bora ni kuweka nyaraka zako kwenye folda ya My Documents na faili zako zingine ambako ziko-mahali pengine isipokuwa desktop. Ikiwa una faili nyingi, unaweza kuziweka kwenye folda tofauti na kuziandika kwa usahihi. Unda njia za mkato “shortcuts” kwenye desktop yako kwajili ya folda au faili unazotumia mara nyingi. Kuboresha maudhui yaliyo kwenye desktop hupunguza matumizi ya operating memory,, hupunguza muda na mzunguko (time and frequency) ambao hutumiwa na hard drive na inaboresha ufanyaji kazi  wa kompyuta yako kwenye programu unazofungua na mambo unayofanya. Tendo rahisi ya kusafisha desktop yakohufanya kompyuta yako kufanya kazi kwa haraka/kasi.

Jinsi ya Kuiweka Safi

Vitu zaidi vya kwenye desktop ndivyo muda mrefu inachukua kompyuta yako kuwaka na kuanza kufanya kazi. Jitihada “kuweka” icons chache kwenye desktop yako. Hatua nyingine unaweza kuchukua ni pamoja na:

  • Futa shortcuts, screenshots au faili ambazo hutumii tena.
  • Kukusanya mafaili yote na folda unayotaka kuyaweka kwenye desktop na badala yake uweke kwenye folda moja kwenye desktop.
  • Ficha icons zote kwenye desktop kwa kubofya kwenye desktop na usichague Show desktop icons kwenye context menu. Rudia mchakato ukitaka kuzionyesha tena.
  •  Tumia Start Menu katika Windows 8 na 10 kama nafasi ya maegesho ya njia za mkato za programu. Unaweza kuPin programu yoyote kwenye skrini yako kwenye Menyu ya Mwanzo (Start Menu) kwa “kuright-click” na kuchagua Pin to Start. Unatakiwa kuweka Menyu yako ya Mwanzo kwa vikundi ili kuweka kila kitu sehemu yake ili kupatikana kwa urahisi.
  • Windows operating systems  nyingi  zinakuja na “desktop cleanup wizard”. Watu wanazipenda au kuzichukia, lakini ni muhimu kuziangalia.
  • Panga ratiba ya kusafisha kwa kila wiki au kila mwezi ili kuondoa vitu vilivyokusanyika kwenye desktop yako tangu ufanye usafi mala ya mwisho.
SOMA NA HII:  Je Kuna Programu ya Windows Unatamani Kuitumia Kwenye Simu ya Adroid ?

Kabla ya kujua, kuweka faili kwenye desktop yako itakuwa kitu cha zamani na kompyuta yako itafanya kazi kama ilivyokuwa mpya.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA