Simu

Unakubali? Windows Kuzipita Android Tablets Ifikapo Mwishoni mwa 2017.

Ingawa Windows inaweza kuwa imekata tamaa kwenye soko la simu, inaonekana kuwa na nafasi ya kupambana katika soko la “tablet” na wachambuzi wanatabiri kwamba Windows inaweza kuzipita tablets za Android ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017.

Ingawa wachambuzi walitafiti kwenye soko la Australia, ukuaji wa kimataifa wa Windows pia umezingatiwa wakati wa kufanya uchambuzi. Inaonekana, watumiaji wengi zaidi wanavutiwa na Windows kuliko Android linapokuja swala la kuchagua tablet.

Kwa mujibu wa taarifa yao:

“Microsoft inaonekana inajikomboa yenye na skrini kubwa za kugusa “touchscreens” licha ya kupoteza vita vya jukwaa la smartphone. Pia, “vifaa vyenye Windows vilivyotokana na wazalishaji mbalimbali vimefaidika kwa kuunganishwa kwa vipengele vya PC na tablet.”

Windows Kuzipita Android Tablets Ifikapo Mwishoni mwa 2017.

Kiukweli , habari hizi zinashangaza ikiwa Google yenyewe inatangaza Chromebooks 2-in-1 juu ya tablets za Android sasa ChromeOS inaweza kutumia apps za Android. Hata hivyo, wachambuzi wamewahi kusema Windows Phone OS itaishinda iOS – sisi sote tunajua jinsi habari hiyo ilivyokwenda.

Kwa hiyo,hili ni swali kwako. Je! Unakubaliana na utafiti? Unapenda kutumia Windows au tablet ya Android?

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kusafisha "Windows Desktop" ili Kuongeza Kasi ya Kompyuta

Zinazohusiana

JIUNGE NA MAZUNGUMZO, TOA MAONI YAKO HAPA

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Lako