Utafiti mpya wa Steam unaonyesha Windows 7 sasa ni OS maarufu zaidi kwa wacheza magemu


Wakati Windows 10 imekuwa OS yenye watumiaji wengi zaidi kwa muda mrefu, miezi michache iliyopita imeonyesha Windows 7 polepole inazidi kutawala. Licha ya hali hii, utafiti wa Steam kuhusu vifaa na programu uliofanyika mwezi Oktoba umeleta data zenye kushangaza sana: mifumo miwili ya uendeshaji ghafla imebadilishana nafasi baada ya watumiaji wa Windows 7 kuongezeka kwa asilimia 22.45 wakati Windows 10 wamepungua kwa asilimia zaidi ya 18.

Ulimwenguni pote, Windows 7 bado ni toleo maarufu zaidi la OS ya Microsoft, lakini ni kwa sababu ya kuwa na idadi kubwa ya watumiaji wa biashara (enterprise users). Taarifa zimekuwa za kweli kwa watumiaji wa Steam; swali ni, kwa nini mabadiliko ya ghafla?

Licha ya nyongeza za faragha zilizotolewa na Microsoft tangu uzinduzi wake, watu wengine bado wanaona jicho la Windows 10 na wana wasiwasi linapokuja swala la kufatilia taarifa za watumiaji. Nchini China, OS imepigwa marufuku kutumika kwenye mifumo ya serikali-Microsoft ilizindua toleo maalum la mamlaka mapema mwaka huu-na watumiaji wengi wa China wanapendelea kubaki kwenye Windows 7.

Windows 10 inaweza kuchukua nafasi ya juu tena kwenye utafiti wa Steam,  hasa ikiwa China itatekeleza tishio lake la kupiga marufuku game ya Battlegrounds kwa sababu ya vurugu nyingi na ubunifu “unaoenda tofauti na maadili ya Kichina na kanuni za maadili.”

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *