Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla amefanya uteuzi wa wajumbe nane kuunda kamati ya kitaifa ya kuandaa mwezi maalum wa maadhimisho ya urithi wa Tanzania (Tanzania Heritage Month).

“Tumeongeza idadi ya wajumbe wa Kamati ya Mwezi wa Urithi wa Tanzania (Tanzania Heritage Month) ili kupata uwakilishi wa Zanzibar na Vijana. Kamati hii itafanya kazi ya kuweka sawa wazo hili na kusaidia utekelezaji wake” amesema Dkt. Kigwangalla.

Kati ya walioteuliwa kuwa wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja mwanamitindo Jokate Mwegelo na muigizaji wa bongo movie Wema Sepetu ambaye hivi karibuni alitangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM) akitokea CHADEMA.

SOMA NA HII:  Wanafunzi wa Primary Tanga kuanza kusoma kwa kutumia Tablet

Inaelezwa kuwa lengo kuu la mwezi huu maalumu ni kunadi utamaduni wa Kitanzania ndani na nje ya mipaka ya nchi ambapo kila kitu kitakuwa cha Kitanzania ikiwa ni pamoja na chakula, michezo, mavazi na ngoma za kiasili na mengineyo.

Taarifa kamili;

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako