Habari za TeknolojiaNyingine

Waziri Mwakyembe: Ni marufuku msanii kuimba nyimbo za siasa [+video]

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Mwakyembe amewasihi wasanii wa Tanzania kuacha kutumiwa na viongozi mbalimbali kwa kuimba nyimbo za masuala ya kisiasa na badala yake wafanye kazi ambazo zitawasaidia kupata mafanikio.

Waziri Mwakyembe aliyasema hayo bungeni wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya wizara yake.

Amesema hakuna mwanamuziki yoyote duniani aliyefanikiwa kwa kuikandia serikali, ametembelea nchi kama Nigeria na wasanii waliofanikiwa kama wakina P Square,Tiwa Savage, Davido ni wasanii wenye mafanikio lakini hawajapata mafanikio hayo kwa kuitukana serikali.

Muziki ni entaritainment industry na sio political Indusrty na hata Afrika Mashariki wasanii kama Chamilione na akina Diamond na Ali Kiba wana mafanikio lakini hawaimbi siasa.
Aidha, waziri alisema kama kuna msanii yeyote anayetaka kuwa mwanasiasa aache muziki akagombee udiwani kwani wasanii waliotaka kuchanganya siasa na muziki walipotea kabisa.

Amemtolea mfano msanii mmoja Fella Ramson Kuti aliyeimba siasa na akaishia pabaya.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *