Wavamizi Mkutano Wa Viongozi Wa CUF, Msajili Ataka Wachukuliwe Hatua


Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi

Baada ya tukio la watu wasiojulikana kuvamia mkutano wa viongozi wa CUF wilayani Kinondoni, kuwapiga na kuwatishia bastola, kabla ya mmoja wao kudhibitiwa na wananchi.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ametaka vyombo vya dola kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika katika vurugu hizo.

Msajili, ni mmoja ya washtakiwa katika kesi iliyofunguliwa na Baraza la Wadhamini wa CUF. Uongozi wa CUF ulitinga Kituo Kikuu cha Polisi kuhoji hatua zilizochukuliwa baada ya shambulio hilo, huku Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad akitoa pole kwa waandishi wa habari na kulaani tukio hilo.

Taarifa ya Jaji Mutungi aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari inasema ofisi yake haitasita kuchukua hatua stahiki kwa vyama vinavyokiuka sheria.

“Nimesoma na kuona katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu vurugu zilizotokea tarehe 22 Aprili, 2017 katika Hoteli ya Vina, Mabibo hapa Dar es Salaam zinazosemekana kuhusisha wanachama wa CUF,” alisema.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA