Watu 10,000 Kunufaika na Mafunzo ya Ujasiriamali na Tehema


Takribani watu 10,000 wanatarajiwa kunufaika katika mradi wa Youth Leadership Program kupitia mafunzo ya Ujasiriamali na Tehema yenye lengo la kuwapa uwezo vijana na wanawake katika kuleta maendeleo ya jamii.

Mradi huo unatekelezwa na shirika lisilo la kiserikali Digital Opportunity Trust (DOT), kwa kutumia njia mtandao umeanza mapema Julai na kutarajiwa kuisha Desemba 2019.

Ujasiriamali na Tehema

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo Meneja Mawasiliano DOT, Ndimbumi Msongole amesema mafunzo hayo maalumu ya kuwajengea uwezo wahitimu wa vyuo mbalimbali ambapo watatumia maarifa watakayo yapata kunufaishia jamii zao kwa mbinu za kibiashara.

“Hakuna malipo ya kupata eimu hii ila vigezo ni kwa wahitimu ambao wanakumbwa na adha ya ajira pindi wanapomaliza chuo hivyo kwa kupitia DOT watanufaika kwa kuweza kujiari na ujuzi wao kuendelezwa kwa asilimia kubwa,”amesema Msongole.

[irp]

Amesema katika mradi huo mikoa inayonufaika kwa sasa ni Dar es salaam, Pwani, na Morogoro lakini wapo katika hatua za mwisho kutoa huduma kwa mikoa ya Dodoma, Mtwara, Kilimanjaro,I ringa na Arusha.

“Tangu kuanzishwa kwa shirika hili ambapo mwaka 2013 tulianza na wahitimu 80 na kwa kupitia wao zaidi ya watu 8000 wamefanikiwa kwa awamu ya kwanza ya utekelezaji,’amesema Msongole.

Mmoja wa wahitimu Yusuph Hamisi amesema kupitia mafunzo hayo kwa sasa amepata ajira ya kuwa mtaalamu wa kompyuta katika taasisi moja hapa nchi huku akiwa anawasaidia wenzake katika kuwapatia mafunzo kama alivyofaidika.

“Napenda kuwaambia vijana wengine wajiunge katika shirika hili lina tija kwa vijana na hakika kupitia mafinzo haya tunaweza kuibafdilisha jamii kwa ujumla,”amesema Hamisi.

Mwakilishi Idara ya Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu,Godfrey Chacha alisema serikali inaunga mkono jitihada zinazofanywa na mashirika haya kwa kuwafikia vijana wengi Zaidi hadi katika ngazi ya vijiji hivyo ni wazi kupitia mitandao wengi watanufaika kwa ajira zinazotolewa na mafunzo pia.

“Serikali haiwezi ikawafikia wote ndio maana inaunga mkono jitihada kama hizi ili kuhakikisha vijana wanakuwa na ujuzi wa ujasiriamali na hata kuapata fursa ya kuzalisha wazo la biashara na kuendelezwa ili kuokoa kizazi kingine,”alisema Chacha.

Alisema licha ya serikali kutoa fedha kwa vijana kwa asilimia tano kwa nagzi ya serikali za mitaa hivyo baada ya kuhitimu mafunzo ni wazi wanaweza wakakopa fedha kwa ajili ya kufanya biashara.

Meneja mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Ubunifu (HDIF),Octavius Kisinda amesema wametenga Sh 1.2 bilioni kwa ajili ya mradi huo ambao kwa sasa ni muendelezo baada ya kufanikiwa kwa kwanza.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA