Sambaza:

Story za wasanii wa sasa kuhusu msoto wa kurekodi nyimbo zao za kwanza ni tofauti sana na story za enzi hizo za kina Juma Nature, Profesa Jay, Dudubaya na wengineo. Zamani shida ilikua ni kurekodi tu, ukifanikiwa kurekodi tayari ustaa unaanza kukujia.

Nyakati zinaenda na Muziki umebadilika sana, mfumo wa soko la muziki wa Tanzania kwa sasa bado sio rafiki kwa wasanii wachanga, ndio maana inatakiwa uwe na heshima na ujitambue ili ufike mbali na kuendana na kasi ya sasa.

Kila msanii anatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili anufaike na kazi yake, muziki wa sasa kipaji chako kinatakiwa kuwa kwenye kiwango cha hali ya juu, ukiwa bora ndio utapata nafasi zaidi ya kutoka na kusikika.

Usiwalaumu media, hii ni biashara, muziki ni biashara na redio na TV ni biashara kitu kinachohitaji ni muziki wa maana. Muziki mzuri wa kuvutia mashabiki na wasikilizaji. Kwa hiyo kaza buti, fanya kazi na wewe ufike level unazotamani kufika na sio kusema kuna ubaguzi kazi ikiwa nzuri ni nzuri tu.

Usisubiri kusaidiwa, wengi wana umoja wa mdomoni lakini mioyoni hawapo hivyo. Kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa nguvu zake, akili yako ndio kitu ambacho kitakufikisha mbali, njiani kuna watu wengi watasema wanataka kukusaidia lakini kumbe wanataka wakutumie tu.

SOMA NA HII:  Mfahamu Mwanzilishi Wa Kampuni ya Simu za Tecno - Tecno Mobile

Usiwe na kinyongo na mtu, haya ni maisha tu, ila jambo la msingi, uvumilivu ni kitu cha muhimu ingawa cha muhimu zaidi ni kuamini kipaji chako bila kujali ni kiasi gani wengine wanakukatisha tamaa kuhusu hicho kipaji chako.

Kila msanii awe mdogo au mkubwa anapenda siku moja anufaike kutokana na mziki wake. Swali la kujiuliza ni una mpango gani kufikia malengo yako ?

Ngoja nikupe ushauri kidogo, kuna njia zaidi ya 3 unazoweza kuzitumia kuwafikia mashabiki wako , njia zinazo msaidia msanii kujulikana nazo ni media kama redio na televisheni, mtandao (blog, tovuti na mitandao ya kijamii) na mtaa kwa mtaa.

Usisubiri na usikae kulaumu media kwa kutokucheza ngoma zako, tumia njia zingine kufikia ndoto zako. Unaweza kuwekeza nguvu nyingi kusambaza nyimbo kupitia “Blog na Tovuti” ili kufikisha kazi zako mtaani.

Mtaa ukielewa utawafanya watu wa media wakutafute maana ikumbukwe kuwa media zipo kwaajili ya watu na watu wanachotaka kuona au kusikia ndicho media zinatafuta.

Hakikisha kabla hujaachia wimbo wako uwe na bajeti nzuri au mtandao wa wadau wa muziki na blogs & tovuti nyingi ili tu wimbo utakapoachiwa usambazwe kila kona.

Kama msanii mchanga utakutana na changamoto kwenye ufanyaji wa kazi ikiwa ni pamoja na kukosa usimamizi mzuri ni vyema ufanye maandalizi mapema na kuwa na mikakati imara ya kukuza sanaa yako.

SOMA NA HII:  Vidokezo 8 rahisi jinsi ya kukuza tukio lako kwenye LinkedIn

Kumbuka kuwa msanii ili awe mkubwa lazima awe mchanga kwanza. Inahitaji uvumilivu na kuwa na subira kufika mbali, muziki wa sasa kipaji chako ni kitu muhimu zaidi na ukijiamini utapa nafasi ya kutoka na kusikika.


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako