Nyingine

Wasanii 5 Wa Kike Wa Kuwaangalia Ndani ya 2017

Inaweza kuwa kweli kwamba Industry ya Muziki wa Tanzania inaleta neema zaidi kwa wasanii wa kiume na kuacha wasanii wa kike wakipenya kwa tabu.

Ila, kwa miaka ya karibuni wasanii kama Vanessa Mdee,Lady Jay Dee na Linah  wamefanikiwa kuonyesha uwezo wao na kwenda sawa na wasanii wa kiume ambao wametawala hii game.

Hii ni list ya wasanii wa kike ambao wanaweza kufanya vizuri zaidi mwaka 2017.

1.Rosa Ree

Anajulikana kama New Rap Queen, Star huyu kutoka lebo ya The Industry inayomilikiwa na Aika na Nahreel ameonyesha uwezo wake na kufanya vizuri na nyimbo kama One Time na Up In The Air.

Kitu kingine kizuri kutoka kwake ni kuwa na Style tofauti ya uimbaji, akiwa chini ya lebo yenye ubora, Rosa Ree ataendelea kushangaza wengi kwenye hii industry .

2.Lulu Diva

Muuza sura kwenye video za Kibongo na msanii mpya wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva kwa sasa ameachia wimbo wake wa pili ‘Usimwache’ ambao video yake imeongozwa na Nicrux kutoka Afrika Kusini. Bado hajaonyesha makali yake kwenye Bongo fleva ila ujio wake unaleta matumaini ya kufanya vizuri siku za mbeleni.

3.Mimi Mars

Ana uwezo wa kuimba, kuandika nyimbo na kufanya utangazaji . Akiwa chini ya Lebo ya Vanessa Mdee, Mdee Music, Mimi Mars ametoa wimbo wake wa kwanza unaitwa Shuga.

Jux amewahi kusema Kuwa Mimi Mars ana uwezo mkubwa wa kuimba kuliko dada yake Vanessa, ingawa ni mapema  sana kusema kwa sasa ila kazi zake na ufikishaji wa sanaa yake ndio itakayomtofautisha yeye na dada yake kwenye soko zima la Bongo Fleva.

4.Maua Sama

Huwezi kumwacha Maua Sama kwenye list hii. Amekuwepo ndani ya game ya bongofleva  kwa muda sasa, anafahamika kwa melody zake tamu kama Sisikii, So Crazy na nyinginezo.

Unaweza kusema ni swala la muda tu Maua atakuwa kwenye A list ya wanamuziki hapa bongo mbali na kipaji alichopewa na mungu , ameonyesha ni kiasi gani muziki una maana kubwa kwenye maisha yake.

5.Chemical

Katika industry ambayo wasanii wa kike wanajulikana zaidi kwa kufanya muziki wa RNB Kwa Chemical ni tofauti, kwa sasa ni moja ya wasanii wanao kuja kwa kasi kwenye industry ya bongofleva.

Chemical ni moja ya wasanii wa kike wachache wanao rap akifuata nyendo za marapa wengine kama chiku keto, Stosh na wengine ambao hata hivyo harakati zao siyo kubwa sana ukilinganisha na marapa wa kiuume.

 

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *