Sambaza:

Nafikiri mimi ni mmoja kati ya watu wachache ambao bado wanavutiwa na Windows Vista, usinihukumu.

Naam, Microsoft hawaipendi na wameweka wazi jambo hilo kwa kusitisha rasmi msaada wake.

Kwanzia sasa, OS inayochukiwa na watu wengi haitapata taarifa yoyote mpya ya usalama, non-security hotfixes, chaguzi zaidi za msaada, au msaada wowote wa kiufundi mtandaoni kutoka Microsoft.

Bila shaka, mtu mwenye PC inayotumia Windows Vista (unatakiwa ku-upgrade ) bado unaweza kuitumia , lakini utakuwa unajiweka karibu zaidi na matatizo ya kiusalama.

M.H .: Mimi hapa nasubiri ujumbe kutoka kwa mtu yeyote ambaye bado anatumia Windows Vista.

SOMA NA HII:  Ripoti : Idadi ya watumiaji wa Intaneti yaongezeka Kufikia milioni 23

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako