Wanapoishi Matajiri Wa Afrika

Comment

Je, umewahi kujiuliza ni nchi gani ya Afrika ina matajiri wengi ? Ukweli ni kwamba kutokana na uchumi wa mataifa mengi ya Afrika kutokuwa imara, nafasi za matajiri wa kiafrika zinazidi kupungua.

Mwaka jana ulikuwa magumu kwa matajiri barani Afrika. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016, kulikuwa na takribani watu 145,000 tu wenye mali zenye thamani ya $ 1 milioni au zaidi wanaoishi barani Afrika. Idadi ilikuwa imeshuka kwa 2% kutoka mwaka uliopita, kwa mujibu wa ripoti ya AfrAsia Bank.

Nchi ya Mauritius, hata hivyo, haikuonyesha tu kupambana na ushukaji wa uchumi ila ilionyesha kuongezeka kwa mamilionea. Idadi ya mamilionea nchini Mauritius ilikua kwa 20% mwaka 2016, kwa 3,800, zaidi kuliko katika nchi kubwa kama Ethiopia na Ghana.

Kwa mujibu wa benki ya Dunia, inachukuliwa kama nchi rahisi barani Afrika kufanya biashara. Kwa kuwa ina viwango vidogo vya kodi huvutia zaidi watu kutoka nje,  nchi hiyo imeunda uchumi wake kuhakikisha inavutia wawekezaji na watalii.

Kwa mfano, watu wanaoishi Mauritius wanaruhusiwa kuwekeza nje ya nchi na hakuna “exchange controls”. Mauritius wameenda mbali zaidi kwa kufungua mipaka yake kwa wageni mwaka 2002, hivyo kuwaruhusu kununua mali moja kwa moja. Wanaponunua kiwanja/nuymba yenye thamani ya $ 500,000, wanakuwa wamepiga hatua ya karibu kupata makazi ya kudumu.

Kwa sasa naishia hapo kuhusu ukuaji wa Mauritius kiuchumi, hizi ni baadhi ya taarifa kuhusu sehemu wanazoishi matajiri wa Kiafrika.

Ni nchi gani ya Afrika ina idadi kubwa ya matajiri Waafrika (Thamani ya $1 million au zaidi);

* Afrika Kusini – 40,400
* Misri– 18,100
* Nigeria – 12,300
* Kenya – 9400
* Angola – 6100
* Morocco – 4600
* Algeria – 4500
* Mauritius – 3800
* Namibia – 3300
* Ethiopia – 3100

Nchi za Afrika zenye ongezeko la matajiri wa kiafrika kutoka 2006-2016;

* Mauritius – 230%
* Ethiopia – 219%
* Rwanda – 107%
* Uganda – 97%
* Kenya – 93%
* DRC – 85%
* Angola – 82%
* Tanzania – 82%
* Ghana – 49%
*Ivory Coast– 45%

Afrika Kusini na Misri bado idadi kubwa ya Waafrika matajiri lakini kwa kuzingatia ukubwa wa Mauritius, nafasi waliyopo inayofaa kupongezwa. Pia wameshika nafasi ya juu kwa kuwa na asilimia kubwa ya ongezeko la matajiri.

Up Next

Related Posts

Discussion about this post

error: Content is protected !!