Wanafunzi wa Primary Tanga kuanza kusoma kwa kutumia Tablet


Katika sherehe zilizofanyika katika kijiji kimoja huko Mkoani Tanga, Mashirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yamegawa tablet zilizowekewa mfumo wa elimu kwa watoto.

Tablet hizo ziligawiwa kama sehemu ya mradi wa majaribio wa miezi 15 chini ya Global Learning XPRIZE ambao ni mradi wa miaka mitano uliotokana na mashindano duniani yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 15.

Mradi huu wa dunia unatoa changamoto kwa timu za wabunifu kubuni na kuandaa zana-wazi za kiteknolojia ili kuwawezesha watoto walio na fursa ndogo ya kupata elimu katika umri wa miaka tisa hadi kumi na mmoja, kujifunza wenyewe stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Kama sehemu ya majaribio, zaidi ya watoto 2,400 kutoka katika vijiji 167 katika wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Mkinga, Muheza, na Pangani watapewa tablet mpya ya aina ya Google Pixel C, Tablet hizo zimewekewa mifumo ya elimu kutoka kwa washindi watano wa mwisho wa Global Learning XPRIZE.

“Teknolojia hii inayowawezesha watoto kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu pasipo msaada wa mwalimu, Msaada utaleta matokeo mazuri katika kuwakomboa watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu.”– Mayasa Hashim Afisa Elimu Mkoa wa Tanga.

“Ubunifu katika teknolojia unaweza kuwa jibu kwa baadhi ya changamoto,majaribio yanamaanisha kwamba tunaweza kutumia teknolojia mpya ili iwahudumie watoto wasio katika mfumo rasmi wa elimu na walio hatarini,” Mwakilishi wa Nchi wa Shirika la WFP Tanzania Michael Dunford.”

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA