Habari za Teknolojia

Wanafunzi kunufaika na elimu ya Papo hapo ya Vodacom

on

Mamilioni ya wanafunzi nchini watanufaika na mpango wa huduma ya elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuongeza ubora na urahisi wa upatikanaji wa elimu hapa nchini mpango huo umeanza kutekelezwa rasmi leo hii na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake inayojishughulisha na shughuli mbalimbali za kijamii”Vodacom Tanzania Foundation”.

Wanafunzi kunufaika na elimu ya Papo hapo ya Vodacom

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa mawasiliano na Vodacom Tanzania Foundation,Rosalynn Mworia alisema wameamua kuleta huduma hii iliyobora kwa wanafunzi itakayojulikana kama Papo hapo ambayo itawawezesha wanafunzi na walimu kupata nakala za masomo bila malipo yoyote na kwa ubora wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza,Kwa kweli tumefarijika sana kwa kuleta huduma hii kwani imekuwa muda mrefu sasa, upatikanaji wa elimu nje ya mfumo wa darasani umekuwa ni mgumu – jambo ambalo limesababisha kizuizi kwa watoto wetu wanafunzi ambao wanataka kupata elimu lakini hawana uwezo wa kuhudhuria darasani.

SOMA NA HII:  Watoto Uingereza kuanza kufundishwa zaidi kuhusu uelewa wa masuala ya digitali

“Shule za papo hapo zitapatikana kupitia mtandao wa Vodacom na huduma hii italenga wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Katika hatua za awali, tutaanza na masomo ya Hisabati na Sayansi na yatakuwa yanapatikana katika lugha za Kiswahili na Kiingereza. Kupitia huduma hii, kutakuwa na upatikanaji wa masomo maalum pamoja na mitihani ya miaka iliyopita, ili kuwasaidia wanafunzi wakati wa maandalizi ya kufanya mitihani. Hii ni fursa kwa wanafunzi wote hususan wale wanaotaka kufaulu masomo ya Hisabati na Sayansi, kufungua akaunti na kuanza kujisomea kupitia elimu ya mtandao bila kuwa na wasi wasi wa malipo”, alisema Mworia .

SOMA NA HII:  Wema Sepetu na Jokate ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii #Tanzania Heritage Month

Mojawapo ya faida kubwa ya shule za papo hapo itaongeza uwezo wa kiteknolojia kwa wanafunzi wanaposoma nje ya muda wa darasani au ndani ya darasa. Pia itawawezesha wanafunzi kupata uzoefu wa mifumo mipya ya kujifunza kwa kuwa huduma itapatikana kwa urahisi kupitia simu za mkononi. Shule za papo hapo zitapatikana pia kwa kutumia kompyuta ikiwa imeunganishwa na mtandao wa Vodacom,Frusa hii ni yakipekee kwa Watu wazima pia waliokosa fursa ya kujiendeleza kielimu kwa sasa wataweza kupata elimu kupitia Shule za papo hapo bila kipingamizi chochote kile,Alisema

Kupitia huduma hii ya Shule za papo hapo, Vodacom Tanzania Foundation imeunga mkono juhudi na jitihada za serikali ya awamu ya tano katika jitihada zake za kuhakikisha kila mtoto wa Mtanzania anapata fursa na uwezo wa kupata elimu bure kuanzia chekechea hadi sekondari.

SOMA NA HII:  Zifahamu pampu za kukamua maziwa ya mama na kuyahifadhi

“‘Mkurugenzi huyo aliendelea kufafanua zaidi ili kurahisisha upatikanaji wake huduma hii, wamehakikisha kuwa huduma ya shule za papo hapo zinapatikana kwenye simu za viwango na bei yoyote alimradi ziwe na uwezo wa kupata mtandao pia slabasi zote za masomo yote zitapatikana na kutolewa kufuata elimu ya kitaifa na kimataifa na waatumiaji wa mara kwanza watatakiwa kujisajili ili kufungua akaunti zao na ndipo wataweza kuendelea na masomo”,

Huduma hii ya Shule za papo hapo kwa sasa inapatikana katika nchi za Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Lesotho, Tanzania, Ghana, Msumbiji na Afrika Kusini tu.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.