Nyingine

Walioshinda nafasi Bunge la EALA hawa hapa, Chadema yatoka patupu

Hatimaye Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania limefanya uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) baada ya mvutano mkubwa na waliofanikiwa kupitishwa ni wabunge saba huku sita kati yaao wakitokea CCM na mmoja CUF.

Wagombea wawili wa Chadema wamepigwa chini baada ya kupigiwa kura za hapana. Wafuatao ndio walioibuka kidedea;

  1. Fancy Nkuhi
  2. Happinness Legiko
  3. Maryam Ussi Yahya
  4. Abdullah Makame
  5. Ngwaru Maghembe
  6. Alhaj Adam Kimbisa
  7. Habib Mnyaa

Mara tu baada ya uchaguzi huo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe amesema hawakubaliani na matokeo hayo na kuahidi kupeleka suala hilo mahakamani.

SOMA NA HII:  80% watashindwa mchezo huu: ni Glass gani itajazwa kwanza?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.