Nyingine

Wakili Aeleza Sababu Za Mbunge Wa Kilombero, Peter Lijualikali Kuachiwa Huru

Mahakama Kuu kanda ya Dar ES Salaam imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali baada ya kukubaliana na warufani kwamba hati ya mashtaka iliyomtia hatiani ilikuwa na upungufu.

Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Jaji Ama- Isaria Munisi baada ya kupitia sababu za kupinga mbunge huyo kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.

Peter aliwakilishwa mahakamani na Wakili Tundu Lissu na Fred Kiwelo wakati Jamhuri ilikuwa ikiwakikishwa na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi.

Mbunge Lijualikali alihukumiwa kwenda Jela Miezi Sita(6) bila faini na Mahakama ya Kilombero. Alikuwa akikabiliwa na Kesi ya kufanya vurugu wakati wa Uchaguzi 2015.

Mmoja wa mawakili waliokuwa wakisimamia rufaa ya mbunge Lijualikali, Fred Kiwelo amesema sababu mojawapo iliyopelekea kuachiwa huru ni pamoja na hati mashtaka kuwa na mapungufu ambapo kosa ambalo alikuwa amehukumiwa nalo limetofautiana na maelezo ambayo amesomewa.

SOMA NA HII:  Kuwa mkweli! Jina gani umetumia ku-save namba ya simu ya mama yako?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.