Home Nyingine Wabunge wa CCM waliopanga kumuona Lema gerezani waitwa wasaliti

Wabunge wa CCM waliopanga kumuona Lema gerezani waitwa wasaliti

0
0


Rais Magufuli amewatisha wabunge CCM kwa kuwaonya vikali, amewashutumu wabunge hao kwa kutoa siri za CCM kwa upinzani na hata kuwagawia wabunge wa upinzani muda wa maongezi bungeni.

Mwenyekiti huyo wa Chama cha mapinduzi ‘CCM’, Rais Magufuli amesema kuwa kuna wabunge wa CCM waliunda kamati ya kutaka kwenda Arusha kumtembelea Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akiwa mahabusu jambo alilosema ni sawa na usaliti kwa chama chake na viongozi wa CCM.

Na mwisho JPM amewapa somo, kwamba anajua kuna njama za kumwondoa Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kwa kutokuwa na imani naye,wakishiriki kwenye mipango hiyo atalirejesha jina la Majaliwa kwa mara ya pili na bunge likilikataa atalivunja na nchi irudi kwenye uchaguzi wa nafasi zote.

Rais amewaambia wabunge wa CCM kuwa yeye ndio aliyekataza bunge lisionakene “live”

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *