Nyingine

Wabunge Kafumu na Kamata, wajiuzulu uongozi kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Dk Dalali Kafumu na makamu wa kamati hiyo Vick Kamata, kwa pamoja wamejiuzulu nafasi zao.

Viongozi hao wameeleza sababu za kuchukua hatua hiyo kuwa ni serikali kuingilia majukumu yao katika utendaji kazi na hivyo wakaeleza kuwa hawaoni sababu za kuendelea na majukumu hayo.

Dr.Kafumu ametoa rai hiyo kwenye kikao cha kwanza cha kamati ya viwanda na biashara kilichoanza leo. Kafumu na Makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Vicky Kamata walipanga kumtembelea Mhe.Godbless Lema gerezani kwa kuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati hivyo wakaitwa wasaliti.

Wamekabidhi barua za kujiuzulu kwenye ofisi ya spika wa bunge jana.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close