Elimu

Top 10 ya vyuo vikuu bora zaidi duniani mwaka 2017

Najua watu wengi mnadhani Chuo Kikuu cha Harvard kilichopo Marekani ndio bora duniani inapotajwa list ya Vyuo Vikuu bora Duniani kwa kuwa kimetoa watu mashuhuri katika fani za Siasa, Sayansi, Tiba na Teknolojia.

Orodha mpya ya kila mwaka ya vyuo vikuu bora zaidi duniani imetangazwa na QS World University Ranking June 9, 2017 ambapo chuo kikuu cha Massachusetts Institute of Technology (MIT) cha Marekani bado kinaongoza.

Vyuo vikuu vya Stanford na Harvard – pia kutoka Marekani – kadhalika vimeendelea kushikilia nafasi ya pili na ya tatu mtawalia. Orodha hiyo ilishirikisha vyuo vikuu karibu 1,000.

Kwa mujibu wa list hiyo Marekani imekuwa kinara kwa kuwa na Vyuo Vikuu bora zaidi ikiwa na Vyuo Vikuu 5 kati ya 10 ambapo ubora wa Chuo hupimwa kutokana na majarida na vitabu vya kisomi vilivyochapishwa, makala zilizonukuliwa, maoni ya wasomi pamoja na waajiri na pia ushiriki wa vyuo vikuu hivyo katika ngazi ya kimataifa.

Chuo kikuu cha Nairobi kimeorodheshwa kuwa kati ya nambari 801 na nambari 1000, kutoka kuanzia nambari 701 hadi 1000 mwaka jana, sawa na Chuo Kikuu cha Makerere.

Vyuo vikuu 10 bora zaidi duniani kwa mujibu wa QS World University Rankings

  1. Massachusetts Institute of Technology (MIT)
  2. Stanford
  3. Harvard
  4. California Institute of Technology (Caltech)
  5. Cambridge
  6. Oxford
  7. University College London
  8. Imperial College London
  9. Chicago
  10. ETH Zurich
SOMA NA HII:  Namna Ya Kuandika Barua Nzuri Ya Kuomba Kazi

 

Inakadiriwa kwamba kwa jumla kuna vyuo vikuu kati ya 20,000 na 26,000 kote duniani.

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako