Vodafone na Nokia kutengeneza mtandao wa 4G kwenye Mwezi


Kampuni maarufu za simu za mkononi Vodafone na Nokia zimetangaza mpango wa kuweka huduma ya mtandao wa 4G kwenye mwezi. Mpango huo unatarajiwa kukamilishwa mwaka 2019.

Mtandao huo utatumiwa na mitambo ya kupeleleza anga za juu kutuma picha, video na maelezo hadi duniani.

“Tunatuma mitambo hii miwili kwenye Mwezi na tutakusanya data, video za HD na picha nyingi zenye maelezo na umuhumu kisayansi. Tatizo ni kwamba hatuwezi kuzituma moja kwa moja kutoka kwa mitambo hiyo hadi duniani. Hii ni kwa sababu itatumia nishati nyingi,” amesema Kate Arkles Gray wa shirika la PTScientists.

“Kwa hivyo, kutumia mtandao wa 4G kwenye Mwezi kutatuwezesha kutuma data, video na picha hizo hadi kwenye mtambo wa kutua kwenye Mwezi ambao una nishati nyingi, na unaweza basi kuvituma hadi duniani.”

“Kwa kufanya hivyo, tutaweza hata kuzitazama video hizo za HD moja kwa moja kutoka kwenye Mwezi tukiwa hapa duniani.

Wengi wameshangaa ni kwa nini kampuni hizo zimeangazia mradi huo badala ya kuangazia zaidi kufikisha huduma ya simu katika maeneo mengi duniani ambayo bado hayana huduma hiyo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA