Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania wiki hii tarehe 19 Agosti 2017 imekuwa mshirika rasmi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Ushirika huo una maana kuwa sasa wateja wanaotumia mtandao wa Tigo watapata nafasi ya kucheza na SportPesa kama ilivyo kwa mitandao ya Vodacom na Airtel.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa kampuni ya SportPesa Ndugu Tarimba Abbas
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa kampuni ya SportPesa Ndugu Tarimba Abbas

Akizungumzia juu ya ushirika huo mpya, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa kampuni ya SportPesa Ndugu Tarimba Abbas alisema “Hii ni nafasi nzuri kwetu na kwa wateja wa Tigo kwani tulikuwa tunapokea maombi mengi juu ya uhitaji wao wa kushiriki kucheza na SportPesa kama ilivyo kwa mitandao mingine.

SOMA NA HII:  Marekani Inasema Korea ya Kaskazini Inahusika na Mashambulizi ya WannaCry

“Wateja wa Tigo wanatakiwa kutuma neno GAME kwenda namba 15888 ili kujisajili, mtumiaji wa mtandao wa tigo ili aweze kucheza na SportPesa anatakiwa kuanza kwa kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kwa kupiga namba *150*01#, kuchagua malipo ya bili, kuweka namba ya biashara ambayo ni 150888, kuingiza namba ya kumbukumbu ambayo ni neno SPORTPESA kisha ataweka kiasi pamoja na namba ya siri ili kumaliza kujisajili”.

Ushirika na Tigo umekuja wakati muafaka ikiwa ni wiki mbili tu tangu kampuni hiyo ambayo ni wadhamini wa vilabu vya Simba, Yanga na Singida United kutambulisha promosheni yake mpya ijulikanayo kama RAFIKI BONUS ambapo wateja wa SportPesa wanapata fursa ya kuwaalika marafiki zao kujisajili na kucheza na SportPesa ili wao waweze kujipatia kiasi cha shilingi elfu mbili za kitanzania (TZS 2000) kwa kila rafiki anayejiunga na kucheza na SportPesa, kwa taarifa Zaidi wanaweza kutuma neno rafiki kwenda 15888.

SOMA NA HII:  Taarifa kutoka TANESCO kuhusu mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya LUKU

Wateja wa SportPesa wanashauriwa kupiga simu za huduma kwa wateja 0764115588, 0658115588 na 0692115588 kwa taarifa zaidi kuhusu bonasi ya rafiki na huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo.

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako