Vitu Vitano (5) vizuri vya kitofauti vinavyopatikana kwenye simu za Samsung Galaxy S8 na S8 Plus


Samsung wametambulisha rasmi simu mpya ya Samsung Galaxy S8 na S8 Plus. Katika ubunifu na utengenezaji wa Samsung Galaxy S8 na S8 Plus Samsung wameenda mbali zaidi kuhakikisha simu hii ni ya kipekee dhidi ya simu zingine zote zilizopo sokoni kwa sasa.

Kama wengi wenu mnavyojua,mfululizo wa simu za Galaxy siku zote zinakuwa daraja la kwanza linapokuja suala la kuendeleza “Flagship” ya simu zao.

Hapa nimekusogezea vitu vizuri vya kitofauti vilivyofanyika katika simu hizi;

Bixby

Kuwa na app yenye uwezo wa kukushauri na kufahamu mambo mbalimbali unayoyafanya katika simu imekuwa ni eneo ambalo kila kampuni ya simu inahakikisha inawekeza kwa sasa. Apple wanayo inaitwa Siri na Google pia wanayo ya kwao na sasa Samsung wamewekeza zaidi. Kwao inaitwa Bixby.

Katika kuelezea upya namna watumiaji wanavyoweza kutumia smartphone zao, Galaxy S8 inakuja na zana ya Bixby. Hii ni sehemu yenye maelekezo ambayo yatawasaidia watumiaji kujua namna ya kuzitumia zaidi simu zao. Utaweza kutumia Kibonyezo kipya cha Bixby kuvinjari kwenye huduma za apps kwa mguso laini, pamoja na mwonekano wa kuwezesha kuandika.

Uwezo wa utambuzi wa mktadha unawezesha Bixby kutoa msaada maalumu unaotokana na uzoefu wa kujifunza mahitaji ya mtumiaji, mahali, na eneo.

Samsung DeX


Samsung DeX ni jibu la kipekee la kubadilisha smartphone yako kwa kukupata huduma sawa na kompyuta yako ya mezani kutoka na kuiongeza Galaxy S8 nguvu za kuchakata na kuleta tija ya hali ya juu,. Watumiaji wa Samsung DeX wanaweza kuona na kusahihisha taarifa kwa kutumia simu zao, na kurahisha ufanyaji kazi wa smartphone kuwa mzuri na wenye kasi.

Bluetooth 5

Simu hizi zimekuwa zimu za kwanza kabisa kuja na toleo jipya la teknolojia ya ya Bluetooth 5. Toleo hili jipya la teknolojia hii inawezesha utumaji wa mafaili haraka zaidi na pia vifaa kama vile spika za bluetooth zinafanya kazi wa ubora na kiwango cha juu zaidi.

Samsung Knox

Galaxy S8 imetumia mfumo wa usalama wa Samsung Knox. Zaidi ya hivyo, Galaxy S8 itatoa uchaguzi wa teknolojia ya utambuzi wa kibaiolojia wa kutambua alama za vidole , jicho, pamoja na uso kwa hali hiyo watumiaji wanaweza kuchagua njia ya uhakiki ya kibaiolojia ambayo inawafaa zaidi.

Ingawa teknolojia hizi zipo tayari kwenye simu nyingi za kisasa ila Samsung ndio wameboresha matumizi yake kwa kiasi kikubwa zaidi.

Utaweza kufunga na kufungua simu, pia utaweza kufunga baadhi ya apps kwa kutumia teknolojia hizo.

Screen (Kioo/Display yake)

Simu za Samsung Galaxy S8 na S8 Plus zinakuja na teknolojia mpya ambayo Samsung wameiita Infinity Display. Kioo chake kimekuja kupinda pande za kushoto na kulia mwa simu. Galaxy S8 inakuja na inchi 5.8 wakati S8 Plus ina kioo/siplay ya inchi 6.2.

Display zake zinatumia teknolojia ya SuperAMOLED, na kiwango cha juu ya HD – QuadHD (2960X1440)

Salama dhidi ya maji na vumbi

Simu zote zinaweza himili kiwango kikubwa cha vumbi na pia kulowanishwa na maji (waterproof).

Pia simu inakuja na teknolojia nyingine mbalimbali za ambazo toleo lake la nyuma pia zilikuwepo kama vile VR, uwezo wa kuchaji wa bila ya kutumia waya n.k.

Hatimaye, simu iliyotarajiwa na wengi ipo mbele yako. Kutokana na sifa zake hapo juu, je, S8 & S8+ zimefikia kiwango unachotaka, au kipo chini?

Kipi kimekuvutia zaidi?

Unaweza kutumia kitufe hapa chini kumshirikisha rafiki yako !

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA