Home Nyingine Vitu mwanaume anavyotakiwa kuwa ameshavifanya akifikia miaka 30

Vitu mwanaume anavyotakiwa kuwa ameshavifanya akifikia miaka 30

0
0

Vijana wengi bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo.

Kama katika umri tulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/mtoto, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili. Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtoto wa kiume lazima uwe ushayatimiza.

1) Kuweka misingi ya kifamilia:

Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia. Kama katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara.

2)Kujitegemea kiuchumi:

Hapa simaanishi kufanya kazi na kupata mshahara pekee, la hasha! Hapa nalenga wale watoto wa mama ambao pamoja na kuwa wana kazi na mishahara, bado wanalalama mishahara haitoshi na kukimbilia kuomba hela nyumbani wanapoishiwa mara kwa mara. Wale ambao bado wanakaa nyumbani hii inawahusu pia. Pia wale wanaotumia 100% ya mishahara kununua vitu vinavyoisha (consumption) wakingoja wapate hela nyingi au wazazi, ndugu na jamaa wawasaidie kwenye uwekezaji. Africa tunachelewa sana kwenye hii sector.

3) Kuwa na kitega uchumi:

Kama unadhani mshahara wako wa milioni kadhaa ni mwingi sana, ngoja augue mtu wa karibu au wewe mwenyewe halafu daktari akuambie mgonjwa wako/wewe ana/unatakiwa ape/upelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi wakati huna bima ya afya inayolipia hilo ndo utajijua kama mshahara wako heshima yake inaishia wapi. Kitega uchumi si lazima uwe na mkampuni mkubwa, la hasha! Ila uwe na kitu cha kueleweka na chenye malengo ya kukua kuwa kitu cha maana. Kwa wale wagumu kuelewa, UNATAKIWA UWE NA PATO LA PEMBENI

4) Makazi:

Uwe hata na kiwanja ! Huezi kunywa bia kila weekend halafu wenzio wakiongelea issues za nyumba/viwanja/mashamba yao unakimbilia kubadilisha mada !

5)Uwe na professional qualification: 

Lazima uwe na defined career (Kama hukubahatika kwenda kidato kingi, uwe na namna ya halali na ya kudumu ya kukupatia kipato). Umri huu kama huna utaalam katika fani yako, jiandae kuwa frustrated ofisini. Madogo wanasoma jamaa angu! Halafu wako tayari kupewa salary ndogo!

6)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea:

Kama wewe ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. Kama umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe.

7) Uwe na busara:

Kama huna busara hadi umri huu basi we sahau!

8) Savings:

Kila mtu ana kipato chake. Ila formula ni kwamba angalau uwe ushahifadhi fedha sawa na mishahara yako ya mwaka na nusu gross of Tax kwa kipindi hicho. Kwa wale wagumu kuelewa, Ukiacha kazi, uwe na uwezo wa kukaa mwaka na nusu bila kuingiza kitu chochote na kuishi maisha yale yale.

9) Umjue Mungu:

Nimeliweka hili mwisho si kwamba ni la mwisho kwa umuhimu, La hasha! Ni ili ulikumbuke zaidi. Kama humuogopi Mungu katika umri huu, basi wewe kwenda Mbinguni ni ngumu kuliko ngamia kupenya tundu la sindani (hata kama ni maskini).

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *