Kompyuta

Vitu 7 vya kuzingatia kabla ya kununua kompyuta

on

Unapofanya maamuzi ya kununua kompyuta ni muhimu sana ufanye maamuzi mazuri kwa sababu jambo hili huwachanganya watu wengi hasa wasiokuwa na uzoefu wa vifaa hivi maana ukifika dukani utakuta za kila namna na miundo tofauti.

Makala ina lengo la kuwasaidia wale wanunuaji wapya wapate muongozo, hapa chini nimeorodhesha mambo kadhaa unayotakiwa kuzingatia kabla ya kununua kompyuta;

1.Mfumo wa uendeshaji (OS) : Windows, Ubuntu (Linux) au Macbook ?
Kitu cha kwanza na cha kuzingatia ni aina gani ya programu endeshi unayohiyaji kuitumia, laptop za Apple ni ghali ukulinganisha na za windows hivyo basi tunashauri kama una bajeti kiasi ni vizuri kununua kompyuta za windows.

Kitu kingine ni aina ya core inashauriwa kutumia laptop yenye icore kuanzia 3 mpaka 7 kumbuka kadri namba inavyopanda ndivyo bei navyo inavyo kuwa kubwa.

2.Diski uhifadhi (Hard Disk)
Diski Uhifadhi ya teknolojia ya SSD, HDD au Hybrid (SSD+HDD) ? kwa watumiaji wa kawaida jambo hili sio muhimu sana ila kwa watumiaji wakubwa wale wanopenda kudownload softwares, movies, games , na wengineo wanahitaji hard disk kubwa. Magwiji wa kompyuta huulizia SATA au SCSI drives.

Ni bora upate laptop inayokuja na diski C ya SSD na diski D ya HDD (yaani Hybrid). Hii itahakikisha unanufaika na ufanisi mzuri zaidi wa programu endeshaji wakati huo huo unapata nafasi kubwa ya ujazo kupitia HDD.

SOMA NA HII:  Fahamu Ukweli Kuhusu KeyBoards

3.Je una matumizi ya aina gani?
Hili ni jambo la muhimu sana kufahamu kabla ya kwenda dukani kununua kompyuta ni vizuri kujua unataka kwa ajili ya matumizi yapi ? kama wewe ni mtumiaji wa kawaida tu (unatumia kwa kazi ndogo ndogo) sio lazima ununue kompyuta yeye specification kubwa, na kwa wale wanao nunua kwajili ya matumizi makubwa, kwa mfano; photoshoping & video editing hawa wanahitaji mashine zenye uwezo mkubwa.

4. Bei
Hapa ndiyo muhimu, utakuta mtu anataka kompyuta yenye sifa kubwa mfano ram Gb 6, au processor quad core, hard disk 500 GB kuendelea halafu unakuta ana kiasi kidogo cha pesa, kama huna hela ya kutosha sio tatizo, nunua kompyuta ya kawaida tu inayoendana na matumizi yako.

5. Random-access memory (RAM)
Kwa watumiaji wadogo hii sio ishu sana, hata ram ya 2Gb ni kubwa kutokana na matumizi kuwa madogo . Ila watumiaji wakubwa hasa wale wanaotumia kompyuta kwa taaluma zao wangependa kutumia kuanzia 4 – 8 GB. Pia operating systems kama windows 32bit na 64bit zina mahitaji yake ya Ram itakayotumika kuziendesha.

6. Ukubwa wa umbo
Baadhi ya watu kama mimi napenda skrini kubwa kama desktop haina kuanzia inch 22 au laptop ianzie inc 15 uwa sina raha. Jambo la muhimu ni kuwa skrini kubwa ni nzuri kwa wale wenye macho yenye udhaifu, ila kuna ambao wanapenda vitu vidogo labda kwa sababu ni rahisi kubeba.

7. Matundu
Kutokana na mahitaji yako, angalia kompyuta ambayo itafaa ukiwa umeweka flash pia unaweza kuweka modem, printer nakadhalika, siku hizi kuna hdmi connection, kuna usb 2 na usb 3 ports na matundu mengine.

Bado kuna vitu vingi vya kuzingatia kama vile jina la kampuni, je ni HP, Dell, Samsung au Toshiba. Pia kuna swala la processor, kuna tofauti kubwa sana kati ya processor za single core kama pentium processors, duo-core, na quad core processors. Tuambie wewe unazingatia vitu gani unapotaka kununua kompyuta ? Toa maoni yako kupitia sehemu yetu ya maoni

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.