Nyingine

Vitu alivyoongea Ruge Mutahaba kuhusu uvamizi wa Makonda Clouds

Baada ya tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia Clouds Tv wakati shughuli za vipindi zikiendelea, leo March 20, 2017  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amezungumzia tukio hilo.

Nimekukusanyia kila kitu alichokizungumza Ruge Mutahaba leo.

Interview ya leo ilipangwa, leo tulikuwa tuzungumzie ishu ya Malkia wa Nguvu, ingawa kuna mengine yametokea hapa katikati’ -Ruge.

Alhamisi asubuhi tulikuwa na kikao na Kamati ya Maudhui TCRA walikuja kutupatia msasa kidogo, akaja Mkuu wa Mkoa Makonda’ -Ruge

Katikati ya kikao Makonda alitutembelea tukaongea mambo kadhaa tukaagana na watu wa TCRA- Ruge

Wakati natoka ofisini nilikutana na Makonda na Vijana wa SHILAWADU nikauliza kwema hapa nikajibiwa ni Story za kawaida tu’-Ruge

Nikiwa kwenye gari alinifata mmoja wa watangazaji wa kipindi cha SHILAWADU kuniambia kuhusu mwanamke aliyezaa na Gwajima -Ruge

Nikawauliza hiyo story mna uhakika nayo mmeibalance mmempata Mchungaji Gwajima? nilimpigia Mkuu wa Vipindi Kerry kumuuliza’-Ruge

Nilitoa maelezo kwa boss wa vipindi CloudsTV kuhusu kipindi kisichokuwa na maana sababu hakija balance na kisiruke hewani’ -Ruge

Saa 10 Alhamisi nilipata Simu ya Gwajima kunieleza kuhusu kuwepo kipindi kinachomuhusu nikamueleza hiyo story haitoruka-RUGE

Nilimueleza Kerry ambaye ni kiongozi awasiliane na Makonda kwamba video yake haitoruka hewani sababu haija balance’ -RUGE

Ijumaa Saa 5 kasoro nilipokea simu kutoka kwa HR wetu kwamba RC Makonda ameingia ofisini akiwa na askari sita wenye silaha -RUGE

Baadaye nilipata simu toka kwa Mkurugenzi Mtendaji Joseph Kusaga kwamba anapewa lawama na RC Makonda tumezuia kipindi chake’-RUGE

Nikaamua kumpigia simu Mkuu wa Mkoa Makonda nikamuuliza ni nini hicho umefanya kwanini hakunipigia mimi kwanza’ -RUGE

Nilipata maelezo kutoka kwa Sam aliyekuwepo mapokezi akanieleza RC Makonda alikuwa anachukua kitu kwenye flash’ -RUGE

Kwa Mara ya kwanza Makonda anatuvunjia heshima sisi kama rafiki zake tulifanya kazi naye vizuri tangu akiwa Mkuu wa Wilaya -RUGE

Ukweli sisi kama chombo cha Habari lazima tujenge heshima ya kutoa habari zenye uwiano lazima tuiheshimu tasnia yetu- RUGE

Hofu yangu ni kwamba kama mimi nipo na mkurugenzi yupo kwanini asingetengeneza mazingira ya kuonana na sisi kwanza-RUGE

Naomba nieleweke wazi hatuwezi kumuacha mtu akatupanda kichwani hii ni dharau kwangu nasimamia watu zaidi ya 200 asinidharau-RUGE

Panapotokea misingi ya hofu lazima tuweke wazi kabisa bila kificho panopohitaji ukweli lazima tuweke wazi ukweli usemwe-RUGE

Mfano wangu ni kwa timu za Simba na Yanga ni mahasimu lakini chombo kinachowasimamia kikiingilia maslahi yao wanaungana -RUGE

Nimefurahi wanaoitwa mahasimu wetu wa Majizo alitupigia simu, Mengi atafika leo kututembelea Tasnia yetu lazima ilindwe -RUGE

Mimi sitaki kuona bunduki mtaani kwa maslahi ya vizazi vya kesho, bunduki ziwepo wanapolinda benki sio kwenye media- RUGE

Tuhukumiwe kama taasisi napenda vijana wapende kutengeneza kesho yao kwa Uhuru lakini sio kwa chuki za kupandikizwa na watu -RUGE

Vijana wa SHILAWADU wapo kwenye hofu wametishwa wamepoteza morali na kazi yao hawana Amani tena wameomba likizo -RUGE

Kwenye uchaguzi wanasema mtu akikufuata kukupa rushwa chukua lakini kura ni maamuzi yako mwenyewe -RUGE

Unakwendaje kutoa kitu kwa mtu asiye na maamuzi na jambo huo utakuwa ni ujinga wako mwenyewe -RUGE

Sisi tunampenda Makonda hatulipi chochote tunaipenda Dar es Salaam tulifanya kampeni ya ‘Dar Mpya’ kwa mapenzi yetu wenyewe -RUGE

Sakata hili lisihusishwe na kutetea vita dhidi ya madawa ya kulevya kama mtu kakosea ni kakosea tu kwa utashi wake -RUGE

Sisi tuna namna yetu ya kuadhibiwa tunahitaji kuwe na Uhuru wa habari, sio kwakua una mamlaka fulani ukatupanda kichwani -RUGE

Viongozi wetu wanapenda kumtaja Mungu lakini matendo yao ni tofauti watu wanaumia kwenye hili -RUGE

Tukiongea kwa watu wanasema tunahitaji mtu atumbuliwe lakini sisi tunaongea kwa nafasi yetu tumeumia kwenye hili -RUGE

Sisi Clouds Media bahati mbaya tumekuwa ni watu wa kuzungumza na watu tunapokosea watu wanatuwajibisha moja kwa moja -RUGE

Nikwambie siri moja Ruge kama ungesema tofauti mimi ningepata tabu sana kufanya kazi CMG kwa nilichokiona mtandaoni-Masoud Kipanya

Suala ni kwamba tulifikiri ni mapungufu ya kibinadamu ina maana Makonda hakujua kuna Camera kila mahali, jambo la kutafakari-RUGE

Hapo kweli ni Clouds, Jumamosi tulidhani anaweza kuomba radhi, na kwenye mitambo ya CCTV kila mtu anapafahamu -RUGE

Makonda ni mdogo wangu sana anaweza kuniomba msamaha, akumbuke mimi nawakilisha kundi la watu waliokosewa kwenye hili -RUGE

Kitu kibaya ambacho kinaumiza moyo RC Makonda ametumia vibaya madaraka yake pamoja na urafiki wake kwetu kama Media -RUGE

Hatua ya maamuzi yetu bado tupo kwenye mashauriano hatutaki kupingana na ajenda za serikali kwa sasa, tutaamua cha kufanya -RUGE

Tulikuwa tunaonekana hiki ni kitu cha Makonda lakini viongozi wengi hawatumii fursa wenye ajenda ya maendeleo waje hapa -RUGE

Sisi sio viongozi ni wananchi tuna miaka 20 kama chombo cha Habari tunakaribisha agenda zenye ubunifu, tujadiliane pamoja -RUGE

Sisi kama Clouds Media tumeumia kuona tukio hili limetokea tena kwa mtu wetu ambaye angeweza kuhoji kwa njia nzuri -RUGE

Toka jambo hili litokee binafsi bado sijafanya mazungumzo yoyote na Mkuu wa Mkoa’ – RUGE

Ni kweli pale Clouds na sijui kaachia nani zile video, Ni kweli tuna Cctv kila sehemu maana hili ni jengo la habari – RUGE

Tusimpe kazi ngumu Rais, huyu baba anatakiwa kuangalia maendeleo yetu, nimesema leo niongelee hili tuendelee na kazi -RUGE

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *