Teknolojia hubadilika mara kwa mara na kila siku kuna mambo mapya yanayovumbuliwa na mitindo pia kubadilika.

Hapa, kuna makala tano kuhusu teknolojia ambazo hazifai kukupita.

1. Li-fi ina kasi mara 100 zaidi ya Wi-fi

Teknolojia mpya ya kutuma data ijulikanayo kama Li-fi imefanyiwa majaribio.

Li-fi ina uwezo wa kumfanya mtumiaji kupata huduma ya mtandao mara 100 zaidi ya Wi-Fi na hutoa kasi ya hadi Gigabait moja kwa kila sekunde. Soma zaidi hapa: Li-fi ina kasi mara 100 zaidi ya Wi-fi

2. Choo kinachojifungua na kujiosha

Choo cha kisasa ambacho kina uwezo wa kujifungua unapokaribia na pia kujiosha, ni moja ya vitu vinavyoonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya teknolojia mpya za bidhaa za elektroniki Las Vegas.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya LG K8 (2017) Bei na Sifa Zake

Choo hicho, kilichopewa jina Neorest, pia humsafisha anayekitumia kwa kifaa kinachotoa maji moto na hewa mtu akiwa ameketi.

Choo hicho kinauzwa $9,800

Kina pia teknolojia inayokiwezesha kuua bakteria na virusi.

Licha ya choo hicho kuuzwa $9,800 (£6,704), waliotengeneza choo hicho vyoo zaidi ya 40 milioni vya miundo ya awali vimeuzwa.

Kampuni ya Toto, iliyotengeneza choo hicho, imesema muundo huo wa sasa bado unaendelea kuboreshwa.

“Huhitaji kuosha bakuli la choo kwa kipindi cha mwaka mmoja,” anasema msemaji wa Toto, Bi Lenora Campos.

3. Je una simu ya Android? Soma utafiti huu

Simu za kisasa zinazotumia mfumo wa Android zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi sana.

SOMA NA HII:  Taarifa kutoka TANESCO kuhusu mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya LUKU

Uchunguzi umebaini kuwa simu zinazotumia mfumo huo zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi mno pasi na kutumia kifaa cha GPS yake.

Aidha simu hizo zinaweza kudukuliwa kwa kutumia matumizi ya betri yake huku utafiti ukisema kuwa simu zinazotumika karibu na kifaa cha kupeperushia masafa ya simu za kuungia mbali.

Simu za kisasa ”Smartphone” hutumia nguvu zaidi inapokuwa mbali zaidi na kifaa hicho cha kupeperushia masafa ya GSM, kwani inachangamoto tele za kungamua masafa.

Matumizi ya nguvu zaidi ya shughuli zingine yanaweza kubaiishwa na ”alogarithm” muundo msingi wa simu yenyewe.

Watafiti hao sasa wameunda mfumo ambao unakusanya habari kuhusu matumizi ya betri ya simu.

SOMA NA HII:  Wema Sepetu na Jokate ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii #Tanzania Heritage Month

‘’Mfumo huo hairuhusu kutumia GPS wala huduma zozote kwa mfano mtandao wa Wi-fi ‘’

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako