Intaneti

Vitu 18 Usivyovijua Kuhusu Mtandao wa Twitter

on

Twitter unaweza kusema kuwa ni jukwaa bora la mtandao wa kijamii kwenye intaneti baada ya Facebook na hapa chini nimekusogezea baadhi ya vitu vya ukweli ambavyo nafikiri unapaswa kuvijua kuhusu mtandao huu wa kijamii.

Twitter

1. Tweet ya kwanza iliyotumwa kwenye Twitter ilitumwa na mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter, Jack Dorsey siku ya tarehe 21 machi, 2006 (mwaka ambao mtandao wa Twitter ulizinduliwa) saa 10:02 jioni. Tweet hiyo ilikuwa na maneno mawili “inviting coworkers”. Angalia hapa  chini

2. Twitter ilianza kupatikana kwa umma Julai 15, 2006.

SOMA NA HII:  YouTube Imeingia Kwenye Deal Kubwa na Label za Muziki

3. Twitter awali ilipangwa kuitwa jina la “stat.us” lakini baadaye ikabadilishwa kuwa “Twttr” na hatimaye, Twitter.

4. Idadi kubwa ya tweets zilizotumwa ndani ya sekunde kwenye Twitter zilikuwa tweets 143,199. Hii ilikuwa tarehe 3 Agosti 2013.

5. Katika siku za kawaida, tweets 6,000 zinatumwa kila sekunde.

6. Tweets milioni 661 zimewahi rekodiwa kama idadi kubwa zaidi ya tweets kwa siku. Kuvunjwa kwa rekodi hii kulichangiwa na Kombe la Dunia la FIFA 2014 lililofanyika mwezi huo.

7. Siku ambayo kulikuwa na tweets chache zaidi kwa siku zilizoandikwa kwenye Twitter zilikuwa tweets milioni 303 (Januari 2016). Wataalam wengine wa teknolijia na takwimu walihusisha kushuka kwa kiwango cha tweets kwa siku na kuanzishwa na kuongezeka kwa umaarufu wa mitandao mingine ya kijamii kama SnapChat na Instagram.

SOMA NA HII:  Tech!! Apps 8 Unazoweza Kuzitumia Kugeuza Windows Pc Kuwa Wi-fi Hotspot

8. Tweets kwa siku zimeongezeka tena na kufikia hadi tweets milioni 500 kwa siku.

9. Kuna kipindi ilichukua miaka 3 kufikisha jumla ya tweets bilioni 1 (Machi 2006 – Mei 2009)

10. Sasa, inachukua takribani masaa 42 (chini ya siku 2) kwa tweets zilizotumwa kufikia bilioni 1.

11. Hadi Januari 2017, Twitter ilikuwa na wafanyakazi zaidi ya 4,000.

12. Twitter ilianzishwa na watu 4: Jack Dorsey, Noa Glass, Biz Stone, na Evan Williams.

13. Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg amewahi kujaribu kuinunua Twitter kwa $500 million.

14. Mpango huo ulivunjika kwa sababu waanzilishi hawakukubali kuuza, na kwa sababu Mark Zuckerberg alikuwa “serious” sana, hakucheka linapokuja swala la utani na alionekana mgumu kujishusha.

SOMA NA HII:  Akaunti ya Twitter ya mwanzilishi wa McAfee VirusScan yadukuliwa

15. Asilimia 21 ya watu kwenye Twitter wapo nchini Marekani.

16. Twitter ina akaunti kama milioni 100 ambazo hutuma tweets kila siku

17.  Marekani ina idadi kubwa ya watumiaji wa Twitter. Brazil inashika nafasi ya pili, ikifuatiwa na Japan, kisha Mexico.

18. Mwisho, watumiaji 80% wanaotembelea Twitter hutumia simu zao za mkononi.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.