Vitu 10 Muhimu Kwa Ulinzi na Usalama wa Kompyuta Yako


Kadri ya siku zinavyosonga mbele teknolojia inakuwa zaidi , kuja kwa programu nyingi mpya za kutumia katika kompyuta na hata vitu vingine vinavyounganishwa na kompyuta ndio matishio mbalimbali ya usalama dhidi ya tarakilishi yako yanazidi kuongezeka toka nyanja mbalimbali za utendaji wa kazi .

Usalama wa Kompyuta

Mfano zamani watu walikuwa wanaogopa zaidi kubadilishana vifaa vya kuhifadhia taarifa kama diski tepe (floppy disk) kwa sababu ya virus baadaye ikaongezeka ujio wa mtandao wa kimataifa unaounganisha tarakilishi ulimwenguni (internet) napo virus na uhalifu mwingine umetokea huko, kwa sasa hivi watu wanatumia simu zao za mikono kuhifadhi taarifa na vitu vingine virus wanahama toka kwenye simu kuingia kwenye tarakilishi au toka kwenye tarakilishi kwenda kwenye simu za mikono na vifaa vingine vya mawasiliano .

Kutokana na visa hivyo hapo juu , kuna njia mbalimbali unaweza kuzitumia kwa ajili ya kuboresha usalama wako unapokuwa kwenye Mindanao na tarakishi yako au unapopokea vifaa vya nje kama flashdisk .

Kitu cha kwanza kujua ni kwamba matishio ya usalama dhidi ya tarakilishi yako na vifaa vyake hutegemea na mazingira ya kazi ya kifaa hicho kwa kila siku au mara kwa mara .

Kwa mfano mtu anayefanyakazi kwenye huduma za sectretarial matishio yake zaidi yapo kwa wale wanaoleta kazi kwa njia ya vifaa vingine kwa ajili ya kuja kufanyiwa kazi na yeye na hapo hapo unakuta kwa muda mrefu hana huduma ya mtandao kwa ajili ya kuboresha programu za tarakilishi yake kama antivirus , firewall na programu nyingine za kufanyia kazi .

Matokeo yake ni kwa tarakilishi hiyo huvamiwa na virus wapya wanaotolewa kwenye mtandao na kuhamishwa kupitia flashdisk kuja kwenye tarakishi yake mara kwa mara na saa nyingine ni pale anaposhindwa kuboresha baadhi ya programu kwa njia ya updates napo programu hizo huleta taabu mbeleni .

[irp]

Yule ambaye anafanyakazi kwenye ofisi zenye tarakilishi nyingi zilizounganishwa kwenye mtandao labda hapo hapo ( LAN ) au wa mbali (WAN ) na matishio yake ni tofauti na yule mchapa karatasi wa steshenari nitaeleza hapa chini .

Ndani ya ofisi unakuta hakuna maelezo ya matumizi ya tarakilishi ( terms of use ) na maelezo mengine kuhusu taratibu za kutembelea mitandao na programu zinazoingizwa kwenye tarakilishi hizo haswa zile zilizounganishwa na mtandao kama ni wa LAN au WAN .

Shida ya kutokuwa na miongozo na maelezo mengine kuhusu matumizi ya tarakishi na mitandao ndani ya maofisi ni kwamba mtu anaweza kuingia na tarakilishi yake binafsi iliyoshambuliwa na wadudu kuja kuunganisha na mtandao wa ofisi na kuleta maradhi kwenye mtandao wa ofisi.

Muda mwingine mtu anaweza kuingia kwenye tovuti za ajabu ajabu akapata madhara huko lakini yeye asione kwa kipindi hicho lakini madhara yakasambaa kwa njia ya mtandao kwenda kwenye tarakilishi za wengine kwa njia ya mtandao kwa kujua au kutokujua.

Mwisho wa siku ni pale mtu kwa kukosa miongozo kuingiza programu zake ambazo haziruhusiswi mwenye tarakilishi yake na kwa wengine ndani ya mtandao wa ofisi matokeo yake ndani ya mtandao wa ofisi kunaweza kutokea tatizo lilisababishwa na hilo na ni ngumu kulimaliza angalau kwa kipindi kifupi

Mtu mwingine ni huyu ambaye hana huduma ya mtandao nyumbani kwake au kazini kwahiyo analazimika kwenda kwenye migahawa ya mtandao yaani “internet café” , kwa uzoefu wangu internet café nyingi haziko salama na ni rahisi kutoa maradhi humo kwenye café na kuyabeba kwa njia ya flash au kwa mtandao kwenda maeneo mengine kwa urahisi zaidi kuliko sehemu yoyote ile

Ndani ya internet café mtu huyu anaweza kuibiwa taarifa zake za benki kama akiombwa kufanya hivyo kutumia tovuti bandia za bidhaa mbalimbali ingawa hii mtu anaweza kufanya hata akiwa kwenye tarakishi yake nyumbani au ofisini au popote pale inategemeanana huduma za ulinzi zilizowekwa kwenye tarakishi hiyo.

Mshauri katika maofisi na sehemu zingine za shughuli kama vyuoni na kwa watoa huduma za mitandao ( ISP ) wengi sio washauri wazuri wanatanguliza fedha mbele kuliko huduma matokeo yake ni kufuata huduma kwa majina au namba kama 2017 na sio ubora wa programu yenyewe kwa kipindi hicho na matishio yaliyokuwemo kwa kipindi hicho

[irp]

Kwa kumalizia naweka vionjo muhimu kwa ulinzi wa tarakilishi yako

  1. Hakikisha unatumia programu unazojua chanzo chake na unapozipata hakikisha leseni zake ni sahihi kwa kudhibitisha usajili wake kwa njia ya mtandao.
  2. Hakikisha tarakilishi yako inaingia kwenye mtandao kwa ajili ya kuboresha programu zako haswa Antivirus au Internet Security angalau masaa 3 kila wiki , unapoboresha programu hizi unakuwa na uhakika wa ulinzi na usalama na kifaa chako kwa asilimia kubwa .
  3. Kuwa na programu nzuri na za kisasa kwenye tarakilishi yako haimaanishi tarakilishi yako haiwezi kufa kesho au kifaa katika mashine hiyo hakiweza kufa kesho au saa hiyo hiyo.
  4. Hakikisha unakuwa na umeme mzuri unaoingia na kutoka ndani ya kifaa chako kwa kuwa na UPS na Stabliser na umeme uko sawa madhara ya kutokuwa na vifaa hivi ni kuharibu vifaa kama powersupply , battery na motherboard au hata kuunguza kabisa .
  5. Kama unatumia sana mtandao kwenye shuguli zako hakikisha una vitu vinavyoweza kukuonyesha ubora wa kurasa za tovuti unazotembelea au kutafuta mara kwa mara ili unapokumbana na tovuti bandia au yenye madhara basi programu hiyo ikupe taarifa mapema . Wakati mwingine zinaitwa viongezeo ( addons ) kwenye browser ( kivinjari ) ingawa sio antivirus zote au internet security zenye huduma hizi lakini kwa sasa ni nyingi zina huduma hizo .
  6. Kuna programu ndogo ndogo zinazoitwa utilities kwa ajili ya kufanya mambo kadhaa kwenye tarakilishi kama kufuta programu , kukagua registry na mfumo mzima wa lina kurekebisha hizi pia ni nzuri sana kwa ajili ya afya ya tarakilishi yako .
  7. Wakati mwingine tarakilishi yako inakuwa na tabia za ajabu ajabu kama kwenda taratibu na kufungua kurasa za mtandao ambazo zinakulazimisha kuangalia mara nyingi hayoni mashambulio ya SPYWARE ni vizuri kuwa na Antispyware ingawa Internet Security nyingi huwa na Antispyware .
  8. Hakikisha programu unazoingiza kwenye tarakilishi yako zinaendana na tarakilishi yako mfano unapotumia Autocad 2011 unatakiwa kuwa na Memory ( RAM) ya angalau GB 3 wewe ukawa na GB 1 ujue utapunguza utendaji wa programu yako hata unapofanya update unaweza kujikuta inakuwa taratibu zaidi hii pia iko kwenye Antivirus na programu nyingine za Kitaaluma .
  9. Hakikisha unazima huduma za wireless au Bluetooth kwenye laptop yako au simu za mikononi haswa unapokuwa sehemu zenye watu wengi na mikusanyiko ya watu kwa ajili ya usalama zaidi ingawa unaweza kuzitumia kwa tahadhari.
  10. Funga ( disable) programu zote zinazosaidia watu kushusha programu au kitu chochote ( download ) moja kwa moja toka kwenye mitandao mbalimbali ukiacha wazi programu hizi ni rahisi kushusha virus na vitu vingine kwa sekunde kadhaa na kudhuru tarakilishi yako .

Kama umeona unashindwa kukagua vichomekwa kwenye tarakilishi yako kama flashdisk kwa njia ya “full scan” basi weka “quick scan” kwa ajili ya kukagua kila kifaa kinachochomekwa kwenye tarakishi yako.

Maelezo haya niliyoyatoa ni zaidi kwa watumiaji wa Operating system za Windows ingawa mengine yanafanana haswa kwenye masuala ya umeme.

Kama una maswali , maoni na maelezo ya nyongeza unaweza kuandika kupitia sehemu ya maoni kwenye mada hii nashukuru kwa kusoma mpaka hapa.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA