Vita ya Facebook na Marekani, Mambo 6 Yanayotarajiwa


Mkurugenzi mkuu wa Facebook, Mark Zuckerberg anakabiliwa na maswali kutoka kwa mabunge yote mawili ya Marekani kuhusu taarifa/ data za kibinafsi hususan zile zinazolenga sakata la Cambridge Analytica – na ni kwa vipi gazeti ndilo lililoweza kugundua uingiliwaji wa mifumo yake.

Haijawahi kutokea nafasi ya kumchambua Zuckerberg ambaye hapatikani kwa urahisi kutokana na kulindwa na kufichwa na kikosi chake cha maafisa wa mahusiano ya umma. Lakini vikao hivyo vya mabunge mawili vilivyopangwa kufanyika Jumanne na Jumatano vitakwenda mbali zaidi.

Atatarajia maswali magumu juu ya uingiliaji wa uchaguzi wa Marekani na hali ya usoni ya mtandao wake wa kijamii wa Facebook. Lakini, haya ni mambo ya kuangalia wakati mmiliki wa facebook akielekea kwenye mabunge ya Congress ya Marekani:

  • Mambo mazuri ambayo Facebook inayaleta duniani.

Jamii , jamii, jamii. Ni neno utakalokuwa ukilisikia sana kutoka kwa Bw Zuckerberg ambaye atafungua kauli zake kwa kusisitizia mazuri ambayo Facebook inayaleta duniani.

Na yuko sahihi. Imeyafanya maisha yetu halisi kuwa kuwa ya bora zaidi , iwe maandalizi ya sherehe ya siku ya kuzaliwa ama maandamano ya upinzani , vimekuwa sana kutokana na Facebook. Kutokana na kwamba unaweza kuwashirikisha wana familia na marafiki picha.

Atazungumzia kuhusu namna Facebook inatumiwa na wafanyabiashara wadogo kote duniani kuwafikia wateja wao haraka, kwa usahihi na kwa gharama ya chini.

Kwa njia iliyo ya moja kwa moja atakuwa amesema msiihukumu sana biashara yangu, kwa sababu kwa kufanya hivyo mnaweza kuwaathiri mamilioni ya watu wengine pia.

  • Atajaribu kuonyesha kuwa mambo ni ya kawaida

Kwa Zuckerberg mwenye umri wa miaka 33 , ambaye anaelewa namna kampuni yake inavyofanya kazi hatakuwa tatizo .Si Mkurugenzi Mkuu anayejificha tu kwenye kumbi za mikutano ya bodi, ana uelewa zaidi kuhusu kampuni yake.

Pia anaweza pia kuelezea masuala ya ndani ya kiufundi ya kamuni yake.

Badala yake , changamoto kwake itakuwa ni kuonekana kwa ubinadamu wake na kukabiliana na majuto – hata kama yeye binafsi moyoni mwake bado anaamini kwamba , kama kampuni ilivyosema awali, watumiaji hao walitoa data/taarifa zao kwa utashi wao.

  • Atamlaumu Kogan

Ni muhimu kukumbuka kwamba wakati Facebook imekiri makosa kuhusina na sera ya taarifa/data na namna ilivyokuwa ikifanya mambo yake kwa usahihi (ama kutokuwa sahini ) katika kujitakasa kwa makosa ya awali , kampuni hiyo imeshikilia kuwa ni Aleksandr Kogan, mtafiti katika chuo kikuu cha Cambridge , mwenye makosa kwa kiasi kikubwa.

Ni Bw Kogan ambaye alibuni programu binafsi ambayo ilikukusanya data ambazo baadae zilidaiwa kutumiwa na Cambridge Analytica . Na ilikuwa Cambridge Analytica ambayo ilisema ilifuta data wakati haikufanya hivyo.

Bw Zuckerberg atajaribu kuonyesha kuwa ni jambo zuri kuhakikisha kuwa wanasiasa wanafahamu mifumo ya Facebook, huku pia akijaribu kutoonekana kana kwamba anawaeleza kuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao.

  • Atahusisha kampuni nyingine

Kwa wakati mmoja kabla ya kusikilizwa kwao , wabunge walitaka wakuu wa kampuni ya Google na Twitter wahojiwe sambamba na Zuckerberg – wakibainisha kuwa maswali mengi yanayowakabili yanawahusu wote.

Kulikuwa na propaganda nyingi za Urusi kwenye Twitter kwa mfano , na mvutano wa YouTube ambao uliorekodiwa na kuhifadhiwa vema.

Hilo halitafanyika sasa. Facebook iko peke yake. Lakini hilo halitamzuwia Bw Zuckerberg kujaribu kuyavuta makampuni mengine ya teknolojia katika mjadala huu, hata kama hatayataja majina

Facebook haikuwa kampuni ya kwanza kutengeneza mabilioni ya dola kutokana na data binafsi na haitakuwa ya mwisho.

  • Majigambo ya kisiasa na maswali mabaya

”Ni Maswali yenye majibu rahisi ya ndio au hapana ,” ni maswali yanaopendwa na wanasiasa katika vikao vya aina hii. Yanafaa zaidi hasa ,pale unapouliza swali ambalo majibu yake ni huwa ni ndio au hapana.

Tarajia kamera kuwaangazia wawakilishi wakati wa kikao hicho, kuwapata wabunge wenye ushawishi zaidi wakiuliza maswali kwa ajili ya kuandaa video za kuwanadi kabla ya kura za nuru ya muhula.

Tarajia bila shaka mmoja wa wabunge kuuliza ” unaweza kuapa hapa leo kwamba Facebook haitauza data za watumiaji? ” – swali ambalo jibu lake litakuwa “bila shaka “. Facebook haijawahi kamwe kuuza data, haitoi kabisa uwezo wa kuzifikia.

  • Mazungumzo yasiyo na mjadala juu ya sheria

Bw Zuckerberg ataelezea kuhusu kipengele kinachoonyesha ukweli juu ya matangazo ya kibiashara – muswada wa sheria ambao utaongeza zaidi uwazi katika matangazo ya kujinadi kwa wanasiasa kwenye mtandao.

Mazungumzo haya yatawarejesha wabunge zaidi kwenye kile kinachoendelea kwenye televisheni , ambako iliwekwa wazi kuhusu nani aliyelipia tangazo la biashara.

Makala hii imeandikwa kwa Msaada wa BBC Swahili

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA