Vita dhidi ya iPhone, Hili ni ​​toleo maalum la Nokia 3310 bei yake ni $ 1,690

Comment

Caviar, wanajulikana kwa kutengeneza “premium smartphones”, sasa wametoa toleo la dhahabu la Nokia 3310. Imepewa jina la Nokia 3310 Supremo Putin, kuipata simu hii itakugharimu $ 1690. Kwa kiasi hicho, unaweza kupata simu 30 za Nokia 3310 .

Nyuma ya simu kuna picha ya dhahabu ya Rais Putin na nukuu kutoka kwenye wimbo wa Taifa wa Urusi. Kwa mbele, kuna kitufe cha dhahabu na picha ya nembo ya Urusi. Muonekano wake ni sawa na simu mpya ya Nokia 3310 iliyotangazwa hivi karibuni kwenye MWC 2017.

Wakati wa kutangaza simu hii ya kifahari, Caviar walitoa kauli hii:

 “We have created a perfect phone for you: sturdy, stylish, expensive, capable of holding battery charge for a long time, and with a loud signal. Sometimes, that’s all one really needs.”

Sina maneno mengine ya kuongezea.

Kama wewe ni tajiri na huna wazo la nini cha kufanya na hela zako, unaweza kutumia kununua Nokia 3310 Supremo Putin Edition hapa.

Unaweza kuangalia simu hii aina ya smartphone Vertu Constellation  (Angalau hii ni smartphone), kama unahitaji utofauti.

Up Next

Related Posts

Discussion about this post