Sambaza:

WhatsApp imeleta njia mpya kwa watumiaji wake wa iOS na Android imetangaza kufanya maboresho ya programu yake pendwa kwa kuweka kipengele kipya ambacho kitamuwezesha mtumiaji wake kutumia aina ya Fonts (herufi) mbalimbali azitakazo.

Vipengele vipya kwenye "WhatsApp status update"

Kipengele kipya kinafanya iwe rahisi kushirikisha Status  kwa ubunifu zaidi pia kipengele kipya cha maandishi kinakuwezesha ku-update mawasiliano yako kwa njia ya kufurahisha na ya kibinafsi.”

WhatsApp imechukua mfumo wa Facebook kwa kuruhusu watumiaji kuweka Status ambapo ataweza kuweka background ya rangi yoyote aipendayo na kisha kuandika chochote akipendacho kwa aina ya muandiko aupendao.

Aina ya herufi za namna tano kwa sasa ndio pekee zinazopatikana pamoja na rangi 22.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno W5 bei na Sifa zake

Pia kwa wale wanaotumia WhatsApp Web (kwenye kompyuta) kwa sasa wataweza badilisha Status moja kwa moja.

Kampuni hiyo pia imetaja  vitu zifuatavyo kuhusu “status updates”:

  • Kudhibiti ambaye anaona Status yako  – Katika mipangilio ya faragha ya WhatsApp (WhatsApp privacy settings), unaweza kuchagua kutoka kwenye machaguo matatu yafuatayo: “my contacts,” “contacts except…” na “only share with…”.
  • Angalia nani amesoma Status yako – Gonga icon ya jicho chini kwenye Status update ili uone orodha ya watu waliosoma status.
  • Jibu Status – Unapoangalia status ya mtu, kuna kitufe cha kujibu, kinakuruhusu kuweka maoni yako kwenye picha yoyote, video, au GIF. Unapojibu, ujumbe wako utatumwa kwenye “WhatsApp chat” na thumbnail ya Status update.
SOMA NA HII:  Njia bora ya kuroot simu yoyote ya tecno bila kutumia kompyuta

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako