Sambaza:

Uchunguzi wa haraka uliofanyika hivi karibuni  ili kupata ufahamu kuhusu kamari ya simu kwa vijana wa Afrika wanaoishi Kusini mwa Jangwa la Sahara umeonyesha kuwa vijana wa Kenya hutumia pesa nyingi kwenye betting ya michezo mbalimbali (takribani Tsh 120000 ) kwa mwezi.

Washirika wao katika nchi nyingine hutumia chini ya dola 50 (takribani Tsh 120000 ) kwa mwezi na wengi wao wanabet mara moja kwa mwezi. Vijana wa Kenya hutumia hela nyingi kwenye bets za soka na wengi hawajawahi kushindi zaidi ya dola 50 za Marekani.

Utafiti huo una matokeo mengine ya kuvutia. Umegawanywa katika “gambling frequency, sports betting na mobile usage”.

1. Gambling frequency

– 54% ya vijana waliofanyiwa utafiti wamejaribu bahati zao katika kamari.

– Kenya ina idadi kubwa zaidi ya vijana ambao wamehusika katika kamari au betting ikiwa na 76% ikifuatiwa na Uganda kwa 57%. Ghana ina idadi ndogo zaidi ya 42%.

– Mzunguko wa kamari ni wa juu kati ya Wakenya ikilinganishwa na Waafrika wengine. Wakati wengine wana-bet mara moja kwa mwezi, Wakenya wengi hutumia mara moja kwa wiki.

2. Sports betting

– Kati ya chaguo maarufu zaidi kwenye kamari, betting ya mpira wa miguu inatawala katika
Nchi zote isipokuwa Afrika Kusini.

– Nchini Afrika Kusini, kurabati (lotteries) ni chaguo la kwanza la kamari ukilinganisha na soka, casino, racing na poker.

SOMA NA HII:  Ukosefu wa Ajira Wasababisha Website ya Chuo Tanzania Kudukuliwa

– Zaidi ya asilimia 79 ya vijana wa Kenya bets zao huziweka kwenye mechi za mpira wa miguu.

3. Mobile usage

– 75% ya wanao bet hufanya hivyo kwa kutumia simu zao za mkononi na Kenya ina idadi kubwa zaidi ya matumizi ya simu kwajili ya kamari ikiwa na 96%.

– Afrika Kusini, ingawa ina kiwango cha juu cha watu kumiliki simu za mkononi Afrika, ina matumizi ya chini ya simu kwajili ya kamari ikiwa na 48%.

“Mobile phones have become the African Las Vegas. Football betting and the popularity of English football leagues continue to grow in a symbiotic way with a growing youth population that continues to be defined by its uptake of technology,” ripoti hiyoninasema.

Iliongezwa, “Although the stakes are not yet high, all the signs are there of a steady and unfettered domination of sports entertainment and gambling in sub-Saharan Africa.”

Uchunguzi huo ulifanya na  GeoPoll mwezi Machi 2017 kwa vijana 3,879 kutoka Kenya, Uganda, South Africa, Ghana, Nigeria na Tanzania kwa kutumia app yao ya simu.


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako