Vifaa vya kiteknolojia

Vifaa 6 vya Teknolojia Ambavyo Kila Mtu Anapaswa Kuwa Navyo

Unaweza kutumia pesa zako kununua kila aina ya vifaa vya ajabu, lengo ni kuwa tofauti. Lakini kuna vifaa vya teknolojia ambavyo hatuwezi kuishi bila kuwa navyo.

Hii ni orodha ya MEDIAHURU ya aina 6 ya vifaa ambazo kila mtu anapaswa kuwa navyo. Pia tumejumuisha mifano michache ambayo tunaipenda.

Wireless headphones nzuri

Jaybird Freedom

Wireless headphones sasa zinapatikana kwa gharama nafuu huku zikiwa na ubora wa sauti na zinakaa vizuri ukizivaa. Angalia BeatsX mpya ya Apple au Jaybird Freedom Wireless, zote mbili zipo imara.

Bluetooth speaker

UE Roll 2

Simu za hivi karibuni zinaweza kupiga sauti nzuri sana, lakini haziwezi kushindana kwa ubora wa sauti kutoka kwenye Bluetooth speaker. UE Roll 2 ni nzuri ukiwa sehemu ya mapumziko kama beach, lakini Bose SoundLink Mini II inatoa sauti nzuri zaidi ndani ya chumba chako cha kulala au jikoni.

Portable smartphone charger

Mophie Powerstation Mini

Ni jambo la kushangaza kutoka nyumbani kwako bila kujua kama betri yako ya smartphone itadumu usiku mzima. Ondoa “wasiwasi wa aina mbalimbali” kwa kumiliki chaja  ya mkononi, kama Mophie Powerstation Mini. Itakupa uwezo wa ziada bila kuhangaika kutafuta sehemu ya kuchajia unapokuwa kwenye mihangaiko yako.

Kamera nzuri

Sony RX100

Ndiyo, pengine kamera ya smartphone yako ni nzuri. Lakini bado ni muhimu kumiliki kamera ya digitali, kama nilivyosema mwanzo. Sony RX100 ni kamera ndogo na nzuri sana, ingawa ni ghali kiasi. Kama unataka ya bei nafuu, jaribu Canon PowerShot 350 HS.

SOMA NA HII:  Je, wanawake wanapuuzwa katika mazingira ya teknolojia ya Tanzania?

Selfie stick

selfie stick

Kama unapenda kupiga selfie basi hii itakufaa, inatoa picha nzuri za kikundi kuliko drone.

Flash drive

SanDisk USB Drive

Licha ya kuongezeka kwa huduma za cloud kama Dropbox na Google Drive, wakati mwingine unahitaji kufuta faili kubwa kutoka kwenye kompyuta moja hadi nyingine. Kwahiyo ni vizuri kuwa na flash drive, siku hizi zinazidi kuwa ndogo na bei yake ni nafuu sana.

Mada zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako