Vidokezo 8 rahisi jinsi ya kukuza tukio lako kwenye LinkedInLinkedIn ni jukwaa kubwa la mtandao wa kijamii ambalo linaweza kuongeza wahudhuriaji wa tukio lako popote pale nchini Tanzania. Kama mjasiriamali, unatakiwa kuitangaza bidhaa yako kwenye jukwaa hili na kuendelea kuwasiliana na wateja wako. Ndiyo sababu, leo, tumekusanya baadhi ya vidokezo bora katika kukuza tukio lako kwenye LinkedIn.

1. Tengeneza LinkedIn Group kwajili ya tukio lako

Kuanzisha LinkedIn group kwa ajili ya tukio lako mwenyewe kunafanya uvutie watu wengi zaidi, wakitaka kupata maelezo zaidi na kuuliza maswali kuhusu tukio lako. Hamashisha ushiriki kwa kujibu maswali na wasiwasi wao. Toa mapendekezo machache, ungana na washiriki wengine, uuliza maswali kwa wasemaji kwenye tukio lako, hivyo ni vitu vichache unavyoweza kufanya.

2. Shirikisha tukio lako kwenye ukurasa wa matukio wa LinkedIn (LinkedIn events page)

Kwenye Ukurasa wako wa Matukio wa LinkedIn, utakuwa na uwezo wa kushirikisha tukio lako. Kichwa cha habari cha tukio hilo ni “clickable” moja kwa moja kuelekea kwenye ukurasa wako. Fikiria kusogeza sehemu hii ya Mradi (Project section) hadi juu ya profile yako wiki moja au zaidi kabla ya tukio hilo. Unaweza pia kuitangaza kwenye Twitter na Facebook ukitumia kiungo (link) ileile. Himiza watu unao husiana nao wabonyeze kitufe cha “I’m Attending” kwenye Ukurasa wa Matukio yako. Hii itaonekana kama “status update” katika LinkedIn connections zao.

SOMA NA HII:  Nunua Simu za Tecno Mtandaoni kupitia ZoomTanzania & Jumia Online Stores

3. Ongea kuhusu tukio lako katika vikundi husika vya LinkedIn

Ni muhimu kuwa sehemu ya LinkedIn Groups ambapo unaweza kuanza kuzungumza juu ya tukio lako, au kumuomba mtu kwenye mtandao wako kukutambulisha! Ukifanya hivyo katika njia sahihi, majadiliano yako yanaweza kuwa maarufu zaidi katika kundi na kupata uonekano zaidi.

4. Weka event teaser kwenye headline yako

Hii inaweza kuwa na ufanisi sana, lakini usifanye hivyo kwa muda mrefu sana. Hakikisha unarejea kwenye kichwa chako cha siku hadi siku (day-to-day headline) baada ya tukio hilo.

5. Andika status

Unaweza kuchapisha sasisho zako (status) kwenye wasifu wako kwa urahisi. Mtandao wako wa shahada ya kwanza utafahamu vizuri. Watu ambao bado wanasita kujiandikisha wanaweza kuvutiwa kujiandikisha kwa njia hii. Mbali na hilo, pamoja na Ukurasa wako wa Kampuni wa LinkedIn, unaweza sasa kuweka status updates ambayo itaonekana kwa wafuasi wako wote kwenye ukurasa wa Kampuni.

SOMA NA HII:  Facebook kufanya utafiti ili kuboresha habari zake

6. Lenga wahusika maalum na ujumbe wa moja kwa moja

Unaweza kuwa na connections 50 tu kwa wakati mmoja kwajili ya kutuma ujumbe wa moja kwa moja. Ujumbe wa moja kwa moja(Direct messages) hutumwa kwenye barua pepe ya mpokeaji na LinkedIn inbox hivyo inaonekana zaidi na ni rahisi kusomwa. Hakikisha unatenegeneza ujumbe wa kibinafsi kwa kila mtu!

7. Pakia (upload) video au PowerPoint presentation ya tukio lako

Maelezo ya tukio haifai kuwa zaidi ya slide moja. Video inaweza kuwa na clip kutoka kwenye tukio la awali au promo kutoka kwa msemaji muhimu.

SOMA NA HII:  Watakaonunua LUKU kwa M-Pesa sasa kulipia

8. Kuza tukio lako kupitia Matangazo

Targeted ads kwenye LinkedIn ni bora katika kukuza tukio lako. Kwanza tambua bajeti yako na tumia LinkedIn Ads Tool au ushirikiane na LinkedIn kwenye mradi maalum, ili kuunda kampeni itakayowavuta watu wengi kwenye tukio lako!

Je, makala hii imekusaidia? Basi like, comment ama share!

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *