Makala

Video nzuri, Ngoma mbovu ni kutwanga maji kwenye kinu

Wimbi la wasanii kuwekeza zaidi kwenye Video na kusahau matayarisho mazuri ya Audio wakiamini video nzuri zitaubeba wimbo linazidi kuongezeka. Wasanii wamekuwa wakiweka nguvu zao zaidi kwenye video bila kuzingatia nguvu ya audio.

Wasanii wengi wamekuwa na mtindo wa kutoa nyimbo mfululizo na kama kawaida yao wanategemea video ziwasaidie. Lakini je, video zimewasadia kwa kiasi gani kuzikuza nyimbo zao?

Msanii anapotoa wimbo utasikia watu wanasema maneno haya baada ya kuusikiliza: “Si mkali lakini ngoja tusubiri video.” Video zinazotoka sasa ni nzuri lakini ukweli ni kuwa tumeshazoea kuona vitu vya aina hii.

Wasanii wameacha kuwekeza nguvu kubwa kwenye kutengeneza muziki zaidi, yaani kuutengeneza muziki wenyewe zaidi kuliko kufikiria video.

Misingi haifwatwi, wamejisahau wakiamini kuwa magari, nyumba za kifahari, sura yenye mvuto na picha zilizopigwa vizuri zinaweza kuwafanya washindane kimataifa.

Nyimbo nyingi zinashindwa kupenya kwenye soko la kimataifa kwa sababu ya Audio mbovu.

Video hata iwe nzuri vipi, kama nyimbo ni mbaya haiwezi kukusaidia kitu, lazima kwanza tutengeneze kazi nzuri ambazo zinapendwa na watu na hazichoshi kusikiliza.

Siku zote muziki mzuri unaishi kuliko hata hizo video, maana unaweza kufanya video kali leo lakini baada ya miaka kadhaa ikawa imepitwa na wakati lakini ukifanya ‘Audio’ nzuri itaendelea siku zote.

Wasanii hawawezi kutoboa kama wanaendelea kutoa Audio Mbovu, lazima tuwekeze pia kwenye audio, Tanzania tunao maproducer wengi wazuri wa kufanya Mastering ni vyema kuwatumie, inashangaza sana video imetayarisha kwa shilingi milioni 40 wakati Audio imetumia shilingi laki mbili pekee.

SOMA NA HII:  Je Thamani Ya Mchezaji Inaweza Kuongezeka Kupitia Mitandao Ya Kijamii?

Turudishe muziki wetu kwenye misingi yake kwamba wimbo mzuri ndio kila kitu. Ni swala la  muda tu mashabiki wataanza kupotezea video kwa kuwa wasanii wanakosa ubunifu na wana  mawazo yanayofanana . Siku hizi hata mwanamuziki ‘underground’ naye anakwenda Afrika Kusini kurekodi video. Imekuwa kawaida sana. Sana.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.