Vanessa Mdee ashirikishwa na na kundi la watayarishaji wa muziki, Major Lazer linaloongozwa na Dj wa Marekani, Diplo

Vanessa Mdee akiwa na Diplo

Vanessa Mdee anaendelea kwenda Juu. Fresh kutoka kutumbuiza kwenye tamasha la muziki la Gidi jijini Lagos, Nigeria wikiendi ya Pasaka, Cash Madame huyo ameonekana kuingia location kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na kundi la watayarishaji wa muziki, Major Lazer linaloongozwa na Dj wa Marekani, Diplo.

Vanessa na Walshy Fire

Kwenye wimbo huo pia member wa Major Lazer, Mmarekani mwenye asili ya Jamaica, Walshy Fire ameshiriki na kuufanya kuwa mradi wa Major Lazer ft. Vanessa. Diplo na Walshy Fire nao walitumbuiza kwenye tamasha la Gidi.

SOMA NA HII:  Nahitaji Antivirus, Je Wewe Unatumia Antivirus Gani Kwenye Kompyuta Yako?

Vanessa ameshare picha kwenye Instagram akiwa location na watayarishaji hao na kuandika:

WORLDWIDE πŸŒŠπŸ‡―πŸ‡² x πŸ‡ΉπŸ‡Ώ x πŸ‡ΊπŸ‡Έ @diplo @walshyfire Happy Easter 😘 #MajorLazer #VeeMoneyIfYouNasty.

Naye Diplo amepost picha kwenye akaunti yake yenye followers milioni 3.5 na kuandika”

US to TZ @vanessamdee.”

Major Lazer linaundwa na members watatu, Diplo, Jillionaire, na Walshy Fire. Ilianzishwa na Diplo na Switch, lakini Switch alijiondoa mwaka 2011.

Vanessa na Walshy Fire

Lakini ni Diplo ndiye mwenye jina kubwa zaidi kwenye kundi hilo na ameshiriki kutengeneza hits za wasanii wengi wakubwa. Kwenye album ya Beyonce, Lemonade, Diplo ametayarisha nyimbo mbili, Hold Up na All Night.

Diplo anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni 26. Major Lazer kumshirikisha Vanessa ni nyundo ya mwisho inayompeleka Vee Money kimataifa moja kwa moja.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Tecno S1 na Bei yake Nchini Tanzania

COMMENTS

WORDPRESS: 0